Picha & Video : MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA SHABIKI WA YANGA SC, BODABODA MAARUFU "SALAMBA D SALAMBA" SHINYANGA MJINI

 
Video: Msafara Msiba wa Shabiki Maarufu wa Yanga SC Salamba D Salamba 

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza katika mazishi ya Katibu wa Klabu ya Yanga FC tawi la Shinyanga Mjini Salamba Daudi Salamba (47) leo Jumatatu Agosti 28,2023 katika makaburi ya Matanda kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.

Salamba D Salamba mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga alikuwa Shabiki Kindakindaki wa Timu ya Yanga, Mtuma Salamu maarufu katika Redio mbalimbali na mwendesha bodaboda maarufu mjini Shinyanga alifariki dunia siku ya Ijumaa Agosti 25,2023 kwa kile kinaelezwa kuwa alikunywa sumu (maji ya betri) kutokana na kuelemewa na madeni ingawa taarifa ya familia inasema alifariki dunia baada ya kuugua ghafla.
R.I.P Salamba D Salamba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post