MKURUGENZI MANISPAA YA TABORA ELIAS KAYANDABILA ACHAGULIWA KATIBU WA ALAT MKOA WA TABORA


Na Mwandishi Wetu, Tabora

MKURUGENZI wa Manispaa ya Tabora Elias Mahwago Kayandabila amechaguliwa kuwa Katibu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Tabora.

Amechaguliwa katika nafasi ya Katibu wa Jumuiya hiyo kwenye kikao cha ALAT Mkoa wa Tabora kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.

Aidha wajumbe wa kikao hicho kwa pamoja kabla ya kikao walitembelea miradi mitatu ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo na kuridhishwa na hatua za utekelezaji.

Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa shule mpya ya Mkoa (Tabora Girls Grand School wenye thamani ya Sh.bilioni 3), ujenzi wa zahanati kwa ufadhili wa TFS na ujenzi wa maduka stendi kuu ya Kaliua.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwa ajili ya shule ya wasichana mkoani Tabora.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post