WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA RASILIMALI ZAO KUTATUA CHANGAMOTO

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Bi.Lilian Liundi akifungua Mafunzo kwa Wakufunzi Wanajamii kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam leo Julai 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam


***************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kutumia rasilimali walizonazo kutatua changamoto walizonazo kuliko kila mara kuilalamikia Serikali kutokufanya jambo fulani wakati wanaweza kutumia rasilimali walizonazo kuleta Maendeleo yao kwa ujumla.

Akizungumza leo wakati akifungua Mafunzo kwa Wakufunzi Wanajamii kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Bi.Lilian Liundi amesema jamii inatakiwa kubainisha rasilimali walizonazo na kuzitumia kwaajili ya kujiletea Maendeleo yao.

"Kwenye jamii zetu kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara hasa kwenye masuala ya maendeleo, jamii imekuwa ikiilalamikia sana Serikali kwamba haijafanya jambo fulani, wakati muda mwingine wanaweza kutumia rasilimali walizonazo kutatua changamoto inayowakabiri". Amesema Bi.Liundi.

Kwa upande wake Bi.Anna Sangai kutoka TGNP idara ya Mafunzo na ujengewaji wa uwezo, amesema mafunzo hayo yatakwenda kuleta mabadiliko hasa jamii kufahamu rasilimali zinazowazunguka na watazitumia kujiletea maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na jamii yao kwa ujumla.

Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Bi.Rehema Mwateba amesema baada ya mafunzo hayo wanategemea kwenye maeneo ambako kumekuwa na uwakilishi, wataenda kuona chachu ya wale ambao wameshiriki mafunzo hayo wanaenda kuleta harakati za kutathimini rasilimali walizonazo kwaajili ya kujiletea maendeleo kwenye maeneo ambayo wanatabainisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Bi.Lilian Liundi akizungumza katika Mafunzo ya Wakufunzi Wanajamii kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam leo Julai 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam Mkufunzi Bi.Rehema Mwateba akiendesha Mafunzo ya Wakufunzi Wanajamii kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam leo Julai 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam.Mafunzo yakiendelea




Wakufunzi Wanajamii kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa Mafunzo yaliyofanyika leo Julai 4,2023 katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post