CHUO CHA MWALIMU NYERERE BUTIAMA KUANZA KUDAHILI OKTOBA 2023


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa chuo hicho Mkoani Mara.


Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kukagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) Mkoani Mara.


Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanga,akitoa salamu za Mkoa wake kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda alipfanya ziara ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT).


Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia Bernard Melau,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kukagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) Mkoani Mara.


Makamu Mkuu wa chuo Utwala Prof Jakson Msafiri ,akitoa taarifa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) Mkoani Mara.



Sehemu ya Watumishi wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati,akizungumza na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa chuo hicho Mkoani Mara.





Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akikagua maandalizi ya ukarabati wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakati wa ziara yake Mkoani Mara.



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa chuo hicho Mkoani Mara.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya ukarabati wa chuo hicho Mkoani Mara.

Na.Mwandishi Wetu-MARA

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kimetakiwa kujielekeza katika kuanzisha Programu zinazoendana na malengo ya uanzishwaji wake.

Agizo hilo limetolewa Mkoani Mara na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati kukagua maandalizi ya ukarabati wa chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kudahili wanafunzi Oktoba 2023 maandalizi ya ujenzi wa Kampasi Kuu ambapo amekitaka chuo hicho kutokuanzisha Programu nyingi kwa haraka zitakazosababisha kuathiri ubora wa elimu.

Prof. Mkenda ametolea mfano wa namna Chuo Kikuu cha Dar es Slaam ambavyo kilianza na Programu moja ya sheria na wanafunzi 12 au 13 na baadaye taratibu kuanza programu nyingine na kuwataka viongozi wa chuo MJNUAT kutokujaribu kuanzisha Programu nyingi na ambazo zinaweza kushusha ubora elimu.

“Tungependa kuona chuo hiki kilichobeba jina la Baba wa Taifa aliyefanya mambo makubwa katika taifa hili kinakuwa bora na chenye umahiri na uwezo wa kutoa wahitimu wenye viwango bora hivyo kuwa moja ya alama inayotambulisha Tanzania kimataifa, ili kufikia azma hiyo lazima kusimamia malengo ya kuanzishwa kwake badala ya kutaka kutoa program nyingi nimefarijika kuwa na mnaaza na programu tatu tu zilizojikita katika masuala ya Kilimo na Teknolojia za kilimo” amesisitiza Waziri Mkenda.

Amesema kuwa hivi karibu kumekuwa na utamaduni wa vyuo vikuu kuanzisha programu nyingi na kudahili wanafunzi wengi jambo ambalo linaweza athiri ubora wa elimu na kuutaka uongozi MJNUAT kudahili wanafunzi kulingana na uwezo wa miundombinu miundombinu iliyopo na kuhakikisha wanaweza kufikiwa moja moja na wahadhiri.

" tumewekeza hapa Takriban Dola za Kimarekani Milioni 44.5 ambazo sawa na shilingi bilioni 108 kupitia mradi wa HEET ili kujenga kampasi kuu . Itakuwa kubwa hivyo mtaongeza wanafunzi ikikamilika". Amesema Mkenda



Mkuu wa Mkoa wa Mara Said Mtanga amesema mkoa utaweka jitihada zake katika kuhakikisha chuo hicho kinakuwa bora na moja ya alama na nembo za kumuenzi Baba wa Taifa

Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini amesema amefarijika kuona mizigo mikubwa ya vifaa kwa ajili ya kuanza ukarabati kwani ni kiashiria Chuo hicho kinakwenda kuanza kudahili wanafunzi huku akiwataka wasimamizi wa ukarabati kuwa na weledi ili kazi hiyo ifanyike kwa ubora na wakati.

Naye Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia Profesa Bernard Mellau amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ametoa zaidi ya shilingi bilioni 2,661 ya kufanya ukarabati na shughuli nyingine tayari kwa udahili

Prof. Mellau ameongeza kuwa ukarabati huo utajumuisha madarasa nane, maabara mbili, bwalo la chakula pamoja na kubadilisha jengo la mikutano kuwa maktaba, kubadilisha nyumba ya mwalimu kuwa zahanati na kuweka viwanja vya michezo

Ameongeza kuwa chuo kitaanza na programu tatu zitakazokuwa kwenye mlengo wa chuo yaani ambao ni kilimo na teknolojia na kwamba tayari Chuo kimeingia makubaliano na Chuo Cha Sokoine cha Kilimo ili kupata Wahadhiri zaidi na Mitaala na kubadilishana uzoefu .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post