UONGOZI WA VIJÀNA KKKT BABATI MJINI WAANDAA MAONYESHO KWA WAJASIRIAMALI

Na Beatrice Mosses - Manyara.

Katika kuelekea wiki ya vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Kati, uongozi wa vijana KKKT Jimbo la Babati, Usharika wa Babati mjini umewataka vijana wajasiriamali kuleta biashara zao na kuzitangaza kanisani hapo.


Akizungumza leo na baadhi ya vijana wajasiriamali kwenye kikao cha maandalizi ya ibada hiyo, Mwenyekiti wa vijana wa usharika wa Babati mjini Christian Bigo, amesema lengo la kuandaa maonyeaho haya ni kuwatangaza vijana wajasiriamali na waumini.


"Lengo letu la kuandaa maonyesho haya ni kuwaleta vijana pamoja lakini pia ni ili vijana tutangaze biashara zetu kwa waumini tunaosali nao ili waweze kutuunga mkono na watutumie kwenye shughuli zote tunazofanya",amesema Bigo.


Naye Katibu wa vijana KKKT Usharika wa Babati mjini Goodluck Leonard amesema kwamba wameamua kutumià fursa hii ya wiki ya vijana ili kuwawezesha vijana wajasiriamali.


"Tuna washarika ambao ni watumiaji wa hiduma zetu làkini hawatujui kwa hiyo tumeamua kuwasogeza vijana pamoja ili waumini watuunge mkono kwa sababu kuna muumini anatamani kusuka lakini hajui akasuke wapi na ndio maana tumeona tutumie wiki hii ya vijana kuwaunganisha vijana na waumini",amesema Leonard.


Maonyesho haya yamepangwa kufanyika Julai 09 mwaka huu ambapo vijana watahudumu kuanzia Ibadani na baadaye kuelekea kwenye maonyesho waliyoyaandaa ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Babati mjini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post