MKUU WA MKOA WA KAGERA AONYA WANAOHATARISHA UHURU NA USALAMA WA TAIFA
Na Mariam Kagenda _ Kagera

Serikali mkoani Kagera imesema  itaendelea kuwachukulia hatua  wale wote  wanaohatarisha uhuru na usalama wa Taifa sambamba na baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaoshiriki  kuandikisha na kuwapa nyaraka mbalimbali za uraia watu ambao sio watanzania.


Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Fatma Mwassa amesema hayo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya  mashujaa iliyotanguliwa na sala ya kuwaombea mashujaa na kutembelea makaburi  ya mashujaa hao waliopigana  vita vya Kagera mwaka 1978_1979  ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika kambi ya Kaboya kikosi cha 21 JWTZ wilaya ya Muleba.

Mhe. Mwassa amesema kuwa  wameisha baini baadhi na wataendelea kuchukua hatua kwani wale wote wanaowaandikisha watu ambao sio watanzania  na kuwapa hati za  kuonyesha kwamba ni  Watanzania ilihali wanajua  sio Watanzania ni raia wa nchi nyingine   hawatohamishiwa vituo vingine vya kazi bali watafukuzwa. 


Ameongeza  kuwa kuna kila sababu na wajibu wa kulinda mipaka  kwasababu Kagera ni mkoa ambao uko mpakani na umepakana na nchi nyingi na kuna mashujaa ambao walifariki kwa kupigania uhuru hivyo serikali haitokubali kuona mtu anachezea amani na anahatarisha usalama wa nchi ya Tanzania.

Amewahimiza wananchi kuendelea kuwaenzi mashujaa hao kwa vitendo na kulinda rasilimali za nchi ya Tanzania na kuwa wazalendo kama ilivyokuwa kwa mashujaa waliojitoa kwa ajili ya nchi yao.

Kwa upande wake askari mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania aliyepigana vita vya Kagera Haidari Issa amesema kuwa moja ya sababu ambayo ilipelekea kushinda vita ni umoja na  mshikamano waliokuwa nao licha ya kuwa walikuwa wanapitia wakati mgumu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post