WAZIRI BASHE AIPA KONGOLE KAMISHENI NA TUME YA USHIRIKA KWA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA SERIKALI



Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.


Na.Alex Sonna-TABORA

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amepongeza Kamisheni na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kutekeleza maelekezo ya serikali na kuja na Mfumo wa kidigitali wa Usimamizi wa Ushirika na kusisitiza Mfumo huo usomane na ule wa kusajili wakulima.

Akizungumza Julai mosi, 2023 mkoani Tabora kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia, Bashe amesema “Tuwe na mfumo mmoja ambao utamsajili mkulima na kuonesha miamala ya mkulima ya kila siku.”

Aidha, amesema serikali imejipanga kuviwezesha viwanda hapa nchini vinavyozalisha mbolea kwa kununua mbolea yote itakayotolewa kwa ruzuku kwa wakulima.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha mbolea inapatikana kwa wakati kwenye msimu wa kilimo na kuondokana na ucheleweshaji uliojitokeza msimu uliopita.

Naye, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amesema Kamisheni itahakikisha inasimamia Ushirika ili kuwa na mabadiliko chanya.

Nsekela amesema wadau wa Ushirika nchini walikutana na kuangalia maeneo saba ambayo ni ukamilishaji wa Mfumo wa Usimamizi wa vyama hivyo utakaofanya shughuli za ushirika zinakuwa kidigitali.

“Kuendelea kusimamia uanzishaji wa Benki ya Ushirika, maamuzi yaliyofikiwa itakapoanzishwa asilimia 51 ya hisa imilikiwe na wanaushirika na asilimia 49 imilikiwe na watu binafsi na mashirika mbalimbali na hadi sasa Shilingi Bilioni sita zimekusanywa na jitihada zinaendelea kuhakikisha zinakamilika kabla ya mwaka huu kuisha,” amesema.

Mwenyekiti huyo amesema wanatilia mkazo vyama hivyo kujiendesha kibiashara na kuwekeza mali zao kwenye uzalishaji.

Kwa upande wake, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege, amesema hadi sasa kuna vyama vya ushirika 7,300 vimeandikishwa na kati yake asilimia 72 ni vyama vya ushirika visivyokuwa vya kifedha.

Amesema asilimia 28 ni vyama vya ushirika vya kifedha na kwenye vyama hvyo kuna wanachama 8,358,326 ikiwa ni ongezeko la wanachama 1, 393, 000 kwa idadi ya waliokuwepo mwaka jana na vimetoa ajira rasmi kwa Watanzania 146,545.

Kuhusu ukaguzi wa vyama hivyo, Mrajis amesema ukaguzi ulibaini changamoto mbalimbali na wameendelea kuchukua hatua na mwaka huu imevunja bodi za vyama 55 ambavyo vilibainika kuwa na tatizo la usimamizi.

Aidha, amesema kuna mashauri 30 yapo chini ya polisi kwa ajili ya uchunguzi na 47 chini ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

“Pia hadi Machi 2023 vyama vya kifedha 780 vimepatiwa Leseni kwa mujibu wa sheria na vina mtaji wa Shilingi Trilioni 1.6 na akiba zenye thamani ya Shilingi Bilioni 803 na Amana zilizofikia Shilingi Bilioni 713.6 huku mali za vyama hivyo zikifikia thamani ya Shilingi Bilioni 945.3,”amesema.

Awali, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Rashid Chuachua, amesema serikali ya Mkoa wa Tabora imehimizwa uwepo wa ushirika wa kisasa unaowajibika kwa wadau kwenye makundi ya uzalishaji mali ya uongezaji thamani mazao na huduma za kilimo.

“Tunashukuru Wizara kwa kuleta wanunuzi wapya wa tumbaku ambao wamechangia uzalishaji kuongezeka,” amesema.



Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Rashid Chuachua,akielezea mkoa wake unavyoshirikiana na wanaushirika wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe.Mariam Ditopile,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege,akitoa taarifa ya ushirika nchini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,akielezea mikakati ya Kamisheni ya TCDC katika kuimarisha ushirika wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Moshi (MoCU) Prof.Alfred Sife,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mhe.Onesmo Buswelu,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe.Kemirembe Lwota,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Katibu Mtendaji wa Shirika la Vyama vya Ushirika (TFC) Bw.Alex Ndikilo,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndg Hassan Makasuvi,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, (TFC) Charles Jishuli,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.


Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (hayupo pichani) ,akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akizindua mfumo wa MUVU wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akikabidhi Tuzo kwa washindi mbalimbali wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia,yaliyofanyika Julai Mosi,2023 Mkoani Tabora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post