
Zifuatazo ni faida 12 kubwa ambazo Tanzania inatarajia kuzipata kutoka na uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam:
1. Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24 tu.
2. Kuongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 hadi kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33;
3. Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka wastani wa siku 4.5 mpaka siku 2
4. Kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 tu kutokana na uboreshaji wa mifumo yạ TEHAMA;
5. Kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka nchi za nje kwenda nchi za jirani, kutoka USD 12,000 mpaka kati ya USD 6,000 na USD 7,000 kwa kasha
6. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33
7. Kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi trilioni 7.76 kwa mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 26.70 kwa mwaka 2032/33
8. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 kwa mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33
9. Maboresho ya magati ya kuhudumia majahazi na abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitali (cruise ships) zitakazo ongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la taifa
10. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer)
11. Uanzishaji wa maeneo huru ya kiuchumi na kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo: sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi; utali; viwanda na biashara
12. Kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.
Chanzo: Takwimu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
Yaani Taifa hili halina viongozi wanaweza kufanya hayo yote?
ReplyDeleteYaani taifa hili halina uwezo wa kuwekeza kwa watu wake kwenye mifumo ya tehama ili walitumikie taifa lao.
Kumbe kelele zote za kuboresha mifumo ya Tehama haijazalisha watu au vijana wanaoweza kutumia tehama kuendesha Bandari zetu? Sasa kama watawala mmeshindwa kuwafanya watu wetu kusimamia raslimali zetu wenyewe mna maana gani kuendelea kuwapo. Halafu hizo faida sasa zimeandikwa kwenye hicho kimeo!!! Au ndio tumeanza kufunika kombe mwanaharamu apite? Kweli Baniani Mbaya, kiatu chake dawa lakini nchi hii, nchi hii, nchi hiii.kuna watu Akili zao zilishashikwa pabaya. Ila na wewe Job Ndugu why? Ulipaona!!!
Tatizo viongozi wote ni wizi ndio ukaona Miradi yote inayosimamiwa na Serekali kuna tatizo mbona husiki Company kama za kina Bakheresa kila kukicha anafunguwa miradi mipya ndio maana Rais Samiha akaamuwa kuleta mabadiliko lkn kuna watu wanapinga wana Sababu zao sio kuitakia mema Serekali
ReplyDeleteYeye Mwenyewe ni Mwizi mwenzao,! Kama sio mwezi alipokea Ripoti ya Cag alichukua hatua gani kwa wanaotuhumiwa!?
DeleteHiyo imepita bila kupingwa wezi,wapigaji,mafisadi na wale wote wasio na chembe ya uzalendo na nchi hii wanywe sumu wajinyonge au wahame watafute nchi nyingine ya kuishi ambayo haitaki wawekezaji
ReplyDeleteUtulivu na hekima ya serikali haya yote yatawezekana na ifike hatua lazma serikali ifanye mamuzi magumu Kwa baadhi ya watu ambao wanatumika vbaya kisiasa ili kuleta taharuki, kama mwekazji atawekeza Kwa faida kubwa kama hii Kwa nchi yetu kwanini wachache wawe mwiba Kwa taifa na serikali kuhusu mabadiliko hayo??, Kwanini tuendelee na mfumo wa kandamixi? Kuna haja serikali ifunge mkanda Kwa ajili TU ya maendeleo ya wananchi, mm naipongeza serikali hii Kwa utulivu,uvumilivu na busara ilyonayo ktk hili, Hakka ingekuwa serikali iliypiita wajingaa na washenzi kama hawa sidhani hata kama wangewaza hata kusogeza mdomo au kucha pale mahakamani, kweli adui wa maendeleo ni sisi wenyewe hasa vibaraka hawa,tunajua wanatumika vibaya nje na chama cha hovyo hapa tz.Tushikamane na serikali, kupitia mabadiliko/mageuzi makubwa kuhusu uwekezaji wa bandari, ifike watz tubadilike na dhana potofu, kusoma siyo kuelimika , bali kusoma ni kuwa mzalendo wa kweli Kwa taifa, serikali/ viongozi, rasilimali, na kutunza tunu za taifa letu.
ReplyDeletePost a Comment