NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AFANYA UKAGUZI WA UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SHINYANGA, ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA ZA MAJI

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog 
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji nchini Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga kwa ajili ya ukaguzi wa utoaji wa huduma za maji mkoani humo.


Ziara hiyo imefanyika jana Julai 20, 2023 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 21 yenye lengo la kukagua ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maji, uendeshaji wa mamlaka za maji na ubora wa utoaji wa huduma kwa wateja mkoani Shinyanga.


Ziara hiyo ilihusisha kutembelea kwenye miradi mitatu ya maji inayotekelezwa ndani ya wilaya ya Kishapu kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA ambayo ni mradi wa maji ya bomba Seseko - Ngundangali, uliogharimu bilioni 2.73 fedha kutoka serikali kuu unaotarajia kuhudumia wananchi wapatao 15,500 kutoka kwenye vijiji vya Seseko, Mpumbula, Ngundangali, Kakola na Dugushilu, mradi wa pili ni mradi wa maji Masanga - Ndoleleji wenye unaogharimu kiasi cha bilioni 2.3 fedha kutoka serikali kuu kupitia Program ya malipo kwa matokeo (Payment for Result) uliousisha ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 100,000 unaotarajia kuhudumia wakazi 12,768 kutoka vijiji vya Ndoleleji, Masanga, Mwampolo na Ng’wang’halanga, mradi wa tatu ni mradi wa ziwa Victoria Iganga - Isagala wenye gharama ya shiringi bilioni 6.62 unaotarajia kuhudumia takribani watu 49,965 katika vijiji 13.


Mara baada ya kutembelea miradi hiyo mitatu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji ameipongeza RUWASA kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kikamilifu na kusema kuwa amelizishwa na ujenzi wa miradi hiyo inayotekelezwa na kuwasihi wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi ili kuharakisha huduma ya maji kwa wananchi.


“Hongereni sana RUWASA kwa kazi hii nzuri mnayoifanya kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kupitia fedha za serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hasani ambapo kwa sasa ametoa Shiringi Bilioni 7 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye wilaya ya Kishapu, tunataka kuona mkoa wa Shinyanga ufike 90% ya upatikanaji wa huduma ya maji ni vyema kulipa madeni ya wakandarasi ili kuwawezesha kumaliza miradi hii ndani ya wakati”, amesema Naibu katibu mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja.


Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo ameipongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha ili kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi.

 “Naipongeza sana serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha nyingi kwaajili ya utekelezaji wa miradi ikiwemo miradi ya maji kutoka ziwa victoria ambapo itakapokamilika tutakwenda kuwa na zaidi ya 90% za upatikanaji wa maji kutoka kwenye 50% zilizopo kwa sasa, ukiangalia katibya vijiji 122 ni vijiji 70 tu ndio vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama ndani ya wilaya hii”, amesema Mbunge Butondo.


Awali akipokea taarifa za mamlaka za maji kwenye kikao cha uwasilishaji wa taarifa za uendeshaji wa huduma za maji mkoni humo KASHWASA, SHUWASA, RUWASA ambapo meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela alisema hadi sasa mkoa wa shinyanga una Vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSOs) vipatavyo 34 ambapo kwa wilaya ya kahama ni 11, Kishapu 9 na Shinyanga 14 ambapo kufikia mwezi Disemba wanatarajia kukamilisha miradi yote inayotekelezwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji nchini Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasili kuanza ziara yake Mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji nchini Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa ziara yake
Mradi wa Tanki la maji Igaga - Isagana.
Mradi wa Tanki la kuhifadhia maji Masanga - Ndoleleji.
Mradi wa maji ya bomba Seseko - Ngundangali.
Meneja RUWASA Wilayani Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo Akizungumza.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Meneja RUWASA Wilayani Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi wilayani humo.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maji nchini Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mara baada ya kupokea taarifa.
Mkurugenzi wa KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na uendeshaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post