BYABATO AWAPUUZA WENYE CHOKOCHOKO, ATAKA WANANCHI WASIKUBALI KUCHONGANISHWA


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv. Steven Byabato akiangalia kitu kwenye simu na Meya wa Manispaa ya Bukoba 
Godson  Gypson (kulia)

Na Mariam Kagenda _ Bukoba

Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv Steven Byabato ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Nishati amesema hatoshindwa kufanya maendeleo katika Jimbo hilo kwa sababu ya chokochoko za watu wachache .

Adv Steven  Byabato amesema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara katika kata ya Kashai iliyopo manispaa ya Bukoba.

Amewahimiza wananchi wa Jimbo hilo kutokubali kuchonganishwa na viongozi wao isipokuwa wawape ushirikiano viongozi  ili watekeleze yale waliyowaaidi na kusisitiza kuwa  kwa kipindi chake cha uongozi atahakikisha Jimbo la Bukoba halikwami kimaendeleo.

Amesema kuwa katika Jimbo hilo viongozi wote kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa wanashirikiana vizuri katika mipango ya maendeleo katika Jimbo hilo  ambapo amesisitiza kuwa Stendi itajengwa,Kingo za mto Kanoni zitajengwa na soko litajengwa.

Ameongeza kuwa  Rais  Samia Suluhu Hassan anawapenda sana wananchi wa Jimbo hilo kwani kuna miradi mingi ya  maendeleo ambayo imejengwa   katika Jimbo hilo ikiwa ni pamoja na miradi ya Afya,Maji , Barabara na elimu .

Naye mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima amesema kuwa uchaguzi uliisha 2020 kwa sasa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM na majukumu yaliyopo ili kuweza kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post