AUAWA KWA KUCHOMWA MKUKI BAADA YA KUFUMANIWA AKIPAKUA ASALI YA MKE WA MTU
Singida. Mkazi wa kijiji cha Merya Tarafa ya Ilongero mkoani Singida, Innocent Dule (49), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa mkuki mgongoni, wakati akifanya mapenzi na mke wa mtu.


Dule anadaiwa kuchomwa mkuki huko mgongoni na Simon Mwangi (58), baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa Mwangi shambani, ingawa muda wa fumanizi hilo haukutajwa.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa, amesema tukio hilo ni limetokea Julai 9, 2023 na mtuhumiwa bado anatafutwa na Polisi.


Kamanda Mutabihirwa amesema japo mtuhumiwa anadaiwa kukimbia kukwepa mkono wa sheria, Jeshi la Polisi wanaendelea kumsaka ili aweze kufikishwa mahakamani na hivyo sheria ichukue mkondo wake.


Taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio, zinadai kuwa mtuhumiwa Mwangi, alipewa taarifa na marafiki zake kuwa mke wake anafanya mapenzi shambani akiwa na Dule (Marehemu), na kwamba ilikua ni kawaida yao kabla ya kuwekewa mtego huo.


(Imeandikwa na Gasper Andrew)

Chanzo _ Joh Media

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post