YANGA MABINGWA ASFC, YAICHAPA AZAM FC 1-0


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuibuka mabingwa kombe la Shirikisho la ASFC kwa kuwachapa wanalambalamba Azam Fc kwa matokeo ya ushindi wa 1-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Mkwakwani Tanga.

Katika mchezo huo, Yanga waliwakosa wachezaji wao wawili muhimu kwenye timu Fiston Kalala Mayele pamoja na Aziz Ki ambao wameitwa kwenye timu zao za taifa,.

Yanga Sc wameweza kushinda mchezo huo wa fainali kwa bao pekee lililofungwa na nyota wao raia wa Zambia Kenned Musonda dakika ya 13 kipindi cha kwanza, bao ambalo limedumu mpaka dakika 90 ya mchezo na kufanikiwa kuibuka mabingwa

Yanga Sc imefanikiwa kuchukua taji hili mara mbili mfululizo na kuendelea kujiwekea rekodi muhimu katika msimu huu ambao wameweza kuvaa medali nne ikiwemo medali kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuingia fainali CAFCC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post