MWANAMKE ATUPWA JELA KWA KUMBAKA NA KUMWAMBUKIZA MAGONJWA YA ZINAA MTOTO WA MIAKA 8

 Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 29 jela Mwanamke wa Kijiji cha Lumuli Desderia Mbwelwa (57) kwa kosa la kumbaka Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na kumsababishia magonjwa ya zinaa.


Siku ya tukio Mwanamke huyo alimkuta Mtoto ambaye ni Mwathirika wa tukio hilo akiwa anachunga ng'ombe kisha akamuuliza wenzake wako wapi na alipojibiwa kuwa wenzake hawapo ndipo akambaka akiwa chini ya mti.


Kesi hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Said Mkasiwa na ilikuwa na Mashahidi watano akiwemo Daktari aliyempima Mtoto na kuthibitisha kuwa Mtoto huyo alikuwa na michubuko na aliambukizwa magonjwa ya zinaa kutokana na kutokwa uchafu eneo la haja ndogo.


Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea, Desderia amesema yeye ni Mtu mzima na kwamba ana Watoto na Wajukuu wanaomtegemea, ndipo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha miaka 29 jela kwa kosa la ukatili wa kingono kwa Mtoto wa miaka 8 pamoja na kumsababishia magonjwa ya zinaa.


Hata hivyo Wakili wake Frank Mwela amesema kuwa anatarajia kukata rufaa kwakuwa Mteja wake hakupimwa ili kubaini kama kweli ana magonjwa hayo ya zinaa, tayari Desderia ambaye ana miaka 57 ameanza kutumikia kifungo hicho cha miaka 29 huku Wakili wake akiendelea kushughulikia taratibu za kukata rufaa.

Chanzo - MillardAyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post