WAZIRI NDUMBARO ATAJA MALENGO SITA KUANZISHWA JUKWAA LA KITAIFA LA HAKI MWANAMKE

WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Damas Ndumbaro,akizungumza wakati akizindua Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri Katiba na Sheria Mhe.Pauline Gekul,wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalum, Mhe.Mwanaidi Ali Khamis,akitoa salamu za Wizara wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Wakili wa Serikali Bi.Ester Msambazi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Meneja Rasiliamali na Mawasiliano kutoka Shirika la Legal Services Facility (LSF) Bi.Jane Matinde,akitoa salamu za Shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa UN Women Bi. Racheal Boma ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Sweden ,Nasieku Kisambu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Aziza Mumba,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria,Dk.Damas Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akizindua Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Damas Ndumbaro,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Jukwaa la Kitaifa la Haki Mwanamake hafla iliyofanyika leo Juni 6,2023 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Katiba na Sheria,Dk.Damas Ndumbaro ameyataja malengo sita ya kuundwa kwa Jukwaa la Haki Mwanamke ikiwemo kupata ushahidi katika masuala yanayoathiri wanawake na changamoto zinazowakabili na kutambua vipaumbele vya haki ya wanawake nchini Tanzania.

Akizunguza leo Juni 6,2023 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo,Waziri Ndumbaro amesema maandalizi ya upatikanaji wa jukwaa hilo umepitia michakato mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na malengo ambayo yatamnufaisha mwanamke moja kwa moja.

Ameyataja malengo hayo ni kupata ushahidi katika masuala yanayoathiri wanawake na changamoto zinazowakabili na kutambua vipaumbele vya haki ya wanawake nchini Tanzania.

Pia,kuwezesha ushiriki mzuri na wa kimkakati juu ya mahitaji ya kimkakati, maslahi na vipaumbele vya wanawake kupata Haki nchini Tanzania.

“Kukuza ubunifu, ujumuishaji na uimarishaji wa uwezo wa pande zote kwa ajili ya kuendeleza majukumu ya mamlaka ya kitaasisi na uendelevu wa Jukwaa,”alisema Waziri Ndumbaro.

Ameyataja malengo mengine ni kukuza mashirikiano yenye maana na msingi na kimkakati kwa Taasisi zenye mlengo sawa na Wizara nchini Tanzania na kwingineko kwa ajili kudumisha upatikanaji wa haki kwa wanawake nchini.

Pia,kuboresha mashirikiano ili kupata, mifano bora na kujifunza miongoni mwa wajumbe wa jukwaa; vi. Kuboresha mifumo ya kisheria, kimazingira, kijamii, kiuchumi ili kuwawezesha wanawake katika Sekta, Taasisi na Mashirika.

“Kukuza na kuimarisha usawa wa usawa kwa wanawake katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa; na viii. Kuhakikisha uzingatiaji wa Hati za Kimataifa na Kikanda kuhusu haki za wanawake,”alisema Waziri Ndumbaro.

Dk Ndumbaro amesema jukwaa la Haki Mwanamke ni jukwaa endelevu ambalo limetengenezewa mifumo imara ya kiutendaji na litajishughulisha na maeneo mbalimbali ya utoaji haki nchini.

Amesema maeneo hayo ni pamoja na eneo la haki kwa mujibu wa sheria, haki za kiuchumi, haki za kijamii, haki za kimazingira na haki za kisiasa.

“ Jukwaa hili litaendeshwa kwa mfumo rasmi ikiwa ni pamoja na kuwa na kamati mbalimbali za kiutendaji, Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Haki Mwanamke, Kamati ya Sekretariati, Kamati ya Uratibu Serikalini na Taasisi zisizokuwa za Kiserikali,”alisema Dk Ndumbaro.

Amesema Serikali katika kulinda haki za Mwanamke itazingatia matakwa ya Katiba, Mikataba ya Kimataifa na Kikanda, Sheria mbalimbali za nchi Kanuni zilizopo, taratibu walizojiwekea na maelekezo mbalimbali ya Viongozi wa Serikali.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalum, Mhe.Mwanaidi Ali Khamis amesema wanawake wamekuwa kimya pindi wanapokumbana na changamoto za maisha hivyo jukwaa hilo litahakikisha wanapata haki zao.

Naye Wakili wa Serikali Ester Msambazi ameeleza kuwa ukatili bado upo kwa wanawake kwakuwa mfumo wa haki haujamwezesha kupata haki kwa wakati hivyo kupitia jukwaa hilo watahakikisha suala hilo linawafikia kwa wakati.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mary Makondo amesema wanawake hukosa haki kwa sababu ya ukosefu wa uelewa hivyo kupitia jukwaa hilo kila mdau atatimiza wajibu wake ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa na wanapata haki zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post