MIGODI YA BARRICK NORTH MARA NA BULYANHULU YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUHAMASISHA JAMII KUPANDA MITI NA KUTUNZA MAZINGIRA


Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara wakishiriki zoezi la kupanda miti katika maeneo ya mgodi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.

                                                       ****
Migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu iliyopo katika wilaya za Tarime na Msalala katika mikoa ya Shinyanga na Mara imeadhimisha Siku ya Mazingira Duniani 2023 kwa wafanyakazi wake kushiriki kupanda miti ya matunda na kivuli, kuhamasisha jamii kupanda miti na kufanya usafi kwenye vitongoji jirani.

Katika maadhimisho hayo, mgodi wa Barrick North Mara umetoa msaada wa miche ya miti ya matunda na kivuli ipatayo 200 na kushirikiana na jamii kuipanda katika Shule ya Sekondari ya Matongo wilayani Tarime.

Akizungumza wakati wa upandaji wa miti hiyo, Meneja Mazingira wa mgodi huo, Frank Ngoloma amesema wameelekeza shughuli hiyo katika shule hiyo mpya ili kuiboreshea uoto wa asili na mazingira kwa ujumla.

“Tumeamua kushirikiana na jamii kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti, tumeanzia ndani ya mgodi ambapo wafanyakazi wa kila idara wameshirikiana na viongozi wao kupanda miti, na hii inaonesha commitment (uwajibikaji) ya mgodi katika kulinda mazingira”,Ngoloma.

Afisa Mtendaji wa Kata (WEO) ya Matongo, Lackson Isibhu, ameupongeza mgodi wa Barrick North Mara kwa kuthamini maadhimisho hayo na kuona umuhimu wa kushirikiana na jamii kupanda miti ili kulinda mazingira.

“Tunaushukuru mgodi wa Barrick North Mara kwa kutambua sikukuu za kitaifa na kimataifa. Kati ya taasisi au mashirika yaliyopo katika wilaya yetu ni Barrick North Mara pekee ndio wanafanya tukio kama hili la siku ya mazingira na wanakuja kusaidiana na jamii kuboresha mazingira,” amesema Lackson.

Kwa upande wake Kaimu Maneja Mahusiano ya Jamii na Mazingira wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Respicius Onesmo, alisema wameamua kuungana na Halmashauri ya Msalala kuhakikisha wanatoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa jamii na mgodi utafadhili zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya vijiji na vitongoji vinavyozunguka mgodi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Charles Fusi, aliipongeza Barrick Bulyanhulu, kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha utunzaji wa mazingira na alitoa wito kwa wananchi kuzingatia utunzaji wa mazingira na kuepuka kuzalisha taka za plastiki ambazo mbali na kuharibu mazingira unasababisha madhara mbalimbali ya Kiafya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, akiongea wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika eneo la Kakola ambapo Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeshirikiana na Halmashauri hiyo kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyahulu uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo ya kitongoji cha Kakola wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyahulu uliopo wilayani Msalala mkoani Shinyanga wakifanya usafi katika maeneo ya kitongoji cha Kakola wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, akikabidhi zawadi ya vifaa vya usafi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa vikundi mbalimbali vya kufanya usafi wilayani humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani jana.
Picha ya Pamoja ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala,Charles Fusi, na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu nyuma ya vifaa vya kuhifadhi taka vilivyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo mbalimbali kabla ya kupelekwa kwenye madampo.
Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara akishiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la shule ya sekondari ya Matongo wilayani humo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara wakiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Matongo wilayani humo baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti katika maeneo ya shule hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani jana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post