Picha : TCRA YAENDESHA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA...."MSITUMIE VISHOKA KUANZISHA VYOMBO VYA HABARI"

Viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa wakipiga picha na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa wakipiga picha na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetoa  Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Kazi na Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo Jumatano Juni 21,2023 katika Ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema lengo kuu la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha waandishi wa habari wanatambua majukumu ya TCRA na kuzijua sheria na taratibu ili wafanye kazi vizuri pamoja kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwashauri na kuwatahadharisha wadau wa mawasiliano wanaotaka kuanzisha vyombo vya habari mfano Redio kuepuka kutumia  watu ambao sio sahihi 'Vishoka' ambao wanawatumia ili kupata leseni kwani wengi wao ni matapeli  badala yake wawasiliane na TCRA ili kusaidia kupata huduma.

"Ni vyema wadau wa Habari wenye nia ya kuanzisha vyombo vya habari mfano vituo vya Radio nchini kuacha kutumia vishoka. Mkitaka kuanzisha radio ndugu zangu fuateni taratibu ambazo TCRA tunaelekeza na muachane na wale Vishoka ambao mwisho wa siku wataishiA kuwaibia tu pesa zenu na mnajikuta mnashindwa kufikia malengo yenu”, amesema Mhandisi Mihayo.

Naye Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Mwanza Press Club na Mwanafunzi wa Sheria amewataka Waandishi wa habari kuzisoma na kuzielewa sheria zilizopo na kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kuepuka kuandika habari za uchochezi na udhalilishaji.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akitoa mada wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta. Kushoto ni Meneja Masoko TCRA Kanda ya Ziwa, Bernadetha Clement, kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akitoa mada wakati wa Semina kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu Majukumu ya TCRA na Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta
Mwezeshaji Edwin Soko akitoa mada kuhusu sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta

Waandishi wa habari Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya TCRA.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blogDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post