MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU KUBORESHA UTENDAJI MIPAKANIKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Prof Joseph Ndunguru amesema Mamlaka hiyo itaboresha mifumo ya Ukusanyaji mapato katika Maeneo ya Mipaka .


Prof Ndunguru ameyasema hayo alipokutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bwana Toba Nguvila mjini Bukoba walipokuwa wakizungumzia namna ya utendaji kazi na uboreshaji wa shughuli za mamlaka hiyo.


Prof Ndunguru amesema Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu itahakikisha inaendelea kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika maeneo yote ya Mipaka ya nchi ikiwemo mkoani Kagera


Ameitaja mipaka hiyo katika mkoa wa Kagera kuwa ni pamoja na Mtukula,Rusumo,Kabanga na Mulongo.


Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa Kagera bwana Toba Nguvila amesema bado kuna changamoto mbalimbali za kiutendaji katika mipaka hivyo kumuomba profesa Ndunguru kuimarisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwenye mkoa huo.


Profesa Ndunguru alikuwa mkoani Kagera kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo mkoani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post