DITOPILE AWAONYA WANASIASA WANAOHUBIRI UBAGUZI, CHUKI SAKATA LA BANDARI





Na Mwandishi Wetu


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile amewashukia wanasiasa wanaotaka kuwagawa Watanzania wanapojadili suala la makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendeshaji wa bandari kadhaa nchini ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam.

Ditopile amesema, miaka miwili ya utawala wa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan umeonesha mafanikio makubwa kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Mbunge huyo amesema hayo kipindi ambacho kuna mjadala unaendelea wa ushirikiano huo kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiujadili kwa misingi wa u-Tanzania Bara na Uzanzibar.

Kutokana na hilo, Ditopile ameibuka akisema,

"Natoa rai kwa wanasiasa wote nchini wanaojadili suala hili la bandari kuepuka kutumia maneno yenye kuibua hisia za ubaguzi, chuki na kuhatarisha amani na mshikamano wetu kama Taifa."

"Ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tumeshuhudia uzalendo wake, nia yake njema kwa Taifa hili na namna anapambana kwa maslahi ya nchi yetu, wanasiasa ni vyema kuweka siasa pembeni tukamuunga mkono Rais Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo."

"Wote ni mashahidi kazi kubwa na nzuri inafanyika awamu hii ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika uwazi wa mikataba na mashirikiano mbalimbali, tunaingia kama Taifa na yote inapitia bungeni kuonyesha nia njema ya Rais Samia Suluhu Hassan," amesema na kuongeza" alisema Ditopile na kuongeza 

"Tupuuze propaganda chafu, siasa za uongo, ubaguzi na fitina. Tusimame pamoja na Rais Samia katika kusimamia maslahi mapana ya nchi yetu. Natoa Rai kwa Watanzania kuwapuuza wanasiasa wanaohubiri siasa za kibaguzi na chuki."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post