MWAKISU AWATAKA WAKIMBIZI NYARUGUSU KUTUNZA MAZINGIRA

Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Isack Anthony Mwakisu amewataka wakimbizi wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu kutunza mazingira sambamba na kupanda miti kwa wingi.

 Ameyasema hayo Leo Juni 5,2023 katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kiwilaya yenye kauli mbiu tokomeza uchafuzi unaotokana na  bidhaa za plastic ambapo amesisitiza kutunza mazingira kwa viwango vya juu kwani ubora wa mazingira ni chanzo cha afya Bora.
 
"Ndugu zangu napenda kusisitiza kuwa hakikisheni mnatunza mazingira haya kwani kufanya hivyo si tu kwa faida ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jamii inayowazunguka bali pia ni kwa ajili ya mtaji wa afya Bora kwenu na familia mlizoanazo,matumizi ya majiko sanifu na mkaa mbadala pia ni suala jema linaliweka mazingira kuwa Safi daima" ,amesema Mwakisu.

Mkuu wa kambi hiyo ya Nyarugusu Bw. Siasa Manjenje amesema kuwa watahakikisha yeye na watumishi wengine ndani ya kambi hiyo wanasimamia kwa kufuata Sheria zote zilizowekwa za utunzaji mazingira kwa wakimbizi kwa mjibu wa Sheria na taratibu za nchi.

Pia baadhi ya mashirika yanayohusika na huduma za kibinadamu (humanitarian) wilayani humo yaliyoshiriki sherehe hizo ni pamoja na UNHCR, Redeso,DRC,CWS,WFP,Save the Children,HelpAge,World Vision pamoja na Goodneighbour.

Sherehe hizo zimeambatana na burudani mbalibali sanjari na mashindano ya mpira wa miguu Kati ya warundi na wakongo huku Warundi wakiibuka kidedea,ngoma kutoka kwa Burundi kikundi cha Mchomoko,brace band ya wakongo pamoja na maonesho ya uoteshaji miti ya asili kwa ajili ya kutunza mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Kanali Isack Anthony Mwakisu
Mkuu wa kambi ya Nyarugusu Bw. Siasa Manjenje

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post