WAFANYABIASHARA MAARUFU 'JAMBO - JAMUKAYA' , GILITU WANG'AKA SAKATA LA BANDARI

Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Bw. Salum Khamis Salum 'Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Bw. Salum Khamis Salum 'Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya amesema wafanyabiashara nchini ndiyo waathirika wakubwa wa Bandari ya Dar es salaam kutokana mizigo yao kuchukua muda mrefu mpaka siku 16 akisisitiza kuwa anatamani kama mkataba wa uwekezaji katika Bandari wangeruhusiwa kuusaini wangekuwa tayari wameshausaini.

Jambo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 20,2023 wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.


“Sisi wafanyabiashara tunaijua bandari kuliko mtu yeyote yule. Sisi ndiyo waathirika wakubwa wa bandari mbovu iliyopo sasa. Mngeturuhusu sisi tungeenda kuusaini huo Mkataba leo. Hii nchi tuna watu wana akili za ajabu, huu siyo mkataba wa kwanza katika Bandari, huu ni mkataba uliofanyiwa marekebisho baada ya wawekezaji waliopita kwenda kwa mtu mwingine”,
 amesema.

“Wafanyabiashara tunauhitaji huu mkataba huu kuliko kitu chochote….Nawashangaa hao wanaopinga mkataba wa uwekezaji, na mkitoka hapo mzungumzie pia Bagamoyo ili kuifungua nchi. Mimi ningeomba nyinyi watu serikali muangalie hao wanaopinga ni akina nani. Sijamuona mimi mfanyabiashara hata mmoja, Wafanyabiashara tunataka makontena yetu yawe yanatoka haraka bandarini, tuyachukue haraka. Tunatumia gharama kubwa kucheleweshewa mizigo yetu bandarini. Hizi gharama za uchelewashaji mizigo sasa zinatosha”,amesema Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Jambo Food Products.

“Sisi wafanyabiashara msituhusishe na wanasiasa, wanasiasa hawana mizigo bandarini, Sisi wenye mizigo tunataka uwekezaji katika bandari, kwani mizigo yetu inachukua mpaka siku 16.Bandari inataka mtu mwenye uwezo”,ameongeza Jambo/Jamukaya.

Kwa upande wake mfanyabiashara maarufu Gilitu Makula amesema amefuatilia na kubaini kuwa wengi wanaopinga uwekezaji katika bandari hawajawahi hata kuwa na kontena bandarini.


“Usumbufu uliopo bandarini ni mkubwa sana. Mkataba huu utasaidia sana mizigo itoke haraka. Hakuna mtu anayetaka kuuza nchi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ni mzalendo. Hawa wanaopinga ni kutafuta umaarufu tu wa kisiasa”,ameongeza Gilitu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema Serikali ipo bega kwa bega na wafanyabiashara na wawekezaji katika kuweka mazingira bora ya biashara ili kukuza uchumi wa nchi. 

"Wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga fanyeni kazi kwa amani. Hakuna biashara itakayofungwa, tufanye biashara kwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za nchi na za biashara zetu. Biashara zitaendelea kama kawaida ili mzunguko wa fedha uendelee kuwepo. Iwe biashara kubwa au ndogo hatutafunga ili kuweza kukuza uchumi wetu", amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Bw. Salum Khamis Salum 'Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukaya akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Group Company Limited, Bw. Salum Khamis Salum 'Salum Mbuzi maarufu Jambo/ Jamukayaakizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 
Mfanyabiashara na Mwekezaji Mkubwa nchini Tanzania Gilitu Makula akizungumza wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alipokutana na kuzungumza na Wawekezaji na Wamiliki wa Viwanda vikubwa na vidogo Mkoa wa Shinyanga. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 
Soma pia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post