ACT WAZALENDO KUTIKISA KAHAMA MJINI, SHINYANGA


Viongozi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga wakizungumza na waandishi wa habari

 Mratibu wa Mkutano wa hadhara Mkoa wa Shinyanga ACT Wazalendo Risasi Semasaba 

 Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Siri Yasini akizungumza na waandishi wa habari

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ACT Wazalendo Nyangaki Shilungushela
Jengo la ofisi ya ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga


Na Shinyanga Press Club

Chama cha ACT Wazalendo kinatarajia  kufanya mkutano wa hadhara katika Manispaa ya Shinyanga na Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga ili kueleza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi wa Mkoa huo pamoja na ufumbuzi wake. 

Hayo yameelezwa leo Juni 03, 2023 na Mratibu wa mkutano wa hadhara Mkoa wa Shinyanga wa Chama cha ACT Wazalendo Risasi Semasaba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Shinyanga amesema Juni 5 mkutano wa hadhara utafanyika Manispaa ya Kahama na Juni 6 itakuwa ni Manispaa ya Shinyanga.

Amesema Juni 6 ni siku ambayo ACT Wazalendo itaeleza ahadi zake kwa wanachama na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga,kutokana na kuendesha shughuli zao kwa utafiti kujua changamoto za Shinyanga ambapo kiongozi  wa ACT Wazalendo  Zitto Kabwe  na viongozi wengine watazungumza na wananchi.

Risasi amesema licha ya Mkoa wa Shinyanga kuwa na rasilimali nyingi yakiwemo madini ya dhahabu na Almasi lakini bado wananchi wa Shinyanga ni masikini wanaachiwa mashimo pamoja na kilimo kushindwa kuwanufaisha wakulima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Siri Yasini amesema wanakuja kuwasha moto Shinyanga kwa kuweka wazi changamoto zilizopo zinazokwamisha maendeleo na kuwataka wananchi kuchukuwa hatua.

Amesema Juni 5 utafanyika mkutano wa hadhara Kahama na Juni 6 uwanja wa Nguzonane Shinyanga Mjini ambapo ACT Wazalendo itakwenda kuweka historia na kuwaomba wananchi kushiriki.

“Hii yote ni kuiona Demokrasia inaanza kufuata mkondo wake,Demokrasia ni kuhakikisha kwamba mawazo chanya yanapatikana hii Tanzania ni ya watu wote hivyo kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha maendeleo yanapatikana”, amesema Yasini.

 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ACT Wazalendo Nyangaki Shilungushela amesema wananchi walikuwa gizani kutokana na vyama vya siasa kunyimwa uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kutoa maoni yao lakini kwa sasa watumie fursa hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments