YANGA SC YACHAPWA 2-1NA USM ALGER FAINALI YA KWANZA CAFCC



*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wao USM Alger ya nchini Algeria baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali ya kwanza CAFCC ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Licha Yanga kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza waliruhusu bao la mapema kupitia kwa mshambuliaji Aymen Mahious dakika ya 32 ya mchezo,bao ambalo liliwapeleka mpumziko USM Alger wakiwa mbele 1-0.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutengeneza nafasi nyingi kwaajili ya kusawazisha bao bila mafanikio hivyo kocha akalazimika kufanya mabadiliko ambayo yalizaa matunda kwa kuwaingiza baadhi ya wachezaji wakiwemo Morisson, Salum Aboubakar, Djuma Shaban na Lomalisa Mutambala ambapowaliweza kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele, goli likitengenezwa na Morisson dakika ya 82.

Baada ya Yanga kupata bao, USM Alger waliweza kuongeza bao dakika mbili mbele kupitia kwa nyota wao Islam Merili dakika ya 84.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments