WADAU WA USAFIRI WA MAJINI KIBITI WAPATIWA ELIMU YA USALAMA, ULINZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 




Na Mwandishi Wetu,Pwani

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania  (TASAC) limetoa elimu ya Usafiri Salama Majini kwa wadau mbalimbali wa wilaya ya Kibiti katika mialo ya Nyamisati Mkoani Pwani Mei 25 mwaka huu

Elimu hiyo iliyotolewa katika mialo iliyozunguka Nyamasati iliwajumuisha wavuvi, manahodha wa vyombo, wamiliki wa vyombo, wafanyabiashara na watumiaji wa vyombo vidogo vya usafiri majini.

Katika utaoji wa elimu hiyo watoa  mada mbalimbali kutoka TASAC, TPA na BMU walitoa elimu ya jinsi ya kutumia vifaa vya uokoaji pindi inapotokea dharura au ajali majini;  utumiaji vifaa vya uokoaji pamoja na matumizi ya kizimia moto (fire extinguisher) na umuhimu wa kuwa na kifaa hicho kwenye vyombo vidogo vya majini.

TASAC imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri majini kutoa elimu katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha wamiliki wa vyombo kuweka vifaa vya kujiokolea lakini pia manahodha na wavuvi kuvaa jaketi okozi wakati wote wawapo safarini au kuendesha shughuli za uvuvi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments