TMRC WAFURAHIA KUORODHESHA TOLEO LA NNE SOKO LA HISA, WIZARA YA FEDHA YATIA NENO

Mgeni rasmi Kamishna wa Usimamizi wa Deni la Taifa Japhet Justin aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dk.Natu El-Maamry (wa nne kulia) akigonga kengele kuashiria uorodheshwaji rasmi kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KAMPUNI ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) imefurahishwa na hatua ya kuorodheshwa kwa hatifungani ya toleo la Nne katika Soko la Hisa la Dar es Salaam huku wakitumia nafasi hiyo kujivunia mafanikio ambayo wamekuwa wakiyapata hasa katika kusaidia katika soko la nyumba nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya TMRC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni Oscar Mgaya amesema Toleo hilo la nne limekuwa na mafanikio kwani wamepata wawekezaji zaidi ya asilimia 32.8 tofauti na walivyokuwa wamepanga.

Amesema hiyo inaonesha wazi kwamba wawekezaji wana imani na taasisi hiyo na ndio maana wamewekeza kwa kiasi kikubwa lakini inaonesha TMRC inatekeleza majukumu yake ya kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia soko la nyumba pamoja na kuendeleza soko la ukuaji wa mitaji

“Kwa hiyo leo ni mara ya Nne tunaorodhesha , kwani huko nyuma kuna tatu ambazo tumefanya na zote zilikuwa na matokeo mazuri, kwa hiyo mpango wetu tunaendelea kutumia soko la hisa na mitaji kuweza kupata fedha za kusaidia soko la nyumba na makazi,”amesema Mgaya.

Kwa upande wake Kamishina wa Deni la Taifa Japhet Justin aliyekuwa amemwakilisha mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dk.Natu El-Maamry amesema hatua hiyo inakwenda kutoa nafasi zaidi ya kuongeza ushawishi wa watu wengi kuingia katika mfumo kama huu wa kuweza kuorodhesha wenzao katika soko la hisa Dar es Salaam.

“Tunashuhudia Toleo la Nne la Hatifungani likiorodheshwa , kwasababu walikuwa na moja, mbili na wakaenda mpaka tatu na leo nit oleo la nne, kwa hiyo niwapongeze kwani wametoka Sh.bilioni 10 mpaka zaidi ya Sh.bilioni 11.28 , nikiwango kikubwa , tunathamini mnachofanya na nimefurahi kushuhudia na kuwa mgeni rasmi.

“Niwapongeze wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hasa nikiwatambua kwa nafasi ya upekee wanahisa wote ambao wamechukua hatinfungani hii ambayo imekwishasema kama asilimia 69 wakiwa wawekezaji mmoja mmoja na kampuni zikichangia asilimia 51

“Kwa hiyo niwapongeze kwa hatua hiyo kubwa, niwapongeze TMRC kwa kuangali fursa ya kusapoti soko letu la nyumba na hawaishi tu njia ya kutafuta mikopo ya muda mrefu lakini wakati huo huo kutumia soko la Hisa la Dar es Salaam kama sehemu muhimu sana ya kupata mtaji wa hatifungani.

“Wanastahili kupongezwa kwa kuwa na muendelezo,mara nyingi tunafanya mara moja lakini wao wameendelea kubaki kwenye malengo yao na niseme tu wanashawishi wenzetu wote kuona waendelee kuona fursa hii kubwa, “amesema.

“Ninafuraha kuona hatifungani inayofuata nimekuwa hapa kwa hiyo tunakwenda mbele katika soko letu la hisa na ndio hamu yetu kuona tunatoa nafasi zaidi ya moja ya watu kupata mtaji, zamani tuliona watu wengi wanapata mikopo kwa kupeana kati ya marafiki na marafiki ,”amesema.

Ameongeza kwa hiyo sekta ya fedha , eneo lao la soko la hisa bado wana nafasi kubwa ya kuwa namba moja na namba mbili kwani wka mujibu wa takwimu wanaongoza mpaka sasa ni zile fedha ambazo watu wanakopeshana binafsi kwa ajili ya kupata mikopo ya kujenga.

“Kwa hiyo naamini fursa hii itakwenda kutupa nafasi zaidi ya kujiamini na kuongeza watu wengi kuingia katika mfumo kama huu wa kuorodhesha wenzao kwa kutumia Soko la Hisa Dar es Salaam ,”amesema.

Ametumia nafasi hiyo kueleza anaamini kadri watu wengi wanavyoingia kwa zaidi ya asilimia 69 wanakwenda kuwezesha watu wengine zaidi kupata mikopo ili wajenge nyumba zao kwa kutumia mfumo huo ambao ni rafiki kwani unatoa muda wa kulipa , hivyo wadau katika sekta hiyo ya utoaji mikopo kwa ajili ya ujenzi wandelee kutoa taarifa zaidi na kuelimish.

“Tuwaambie watu tunaweza kujenga nyumba sio kwa namna moja tu ya kusema niwe na pesa yangu nije nijenge nyumba lakini wakati mwingine ninaweza kujenga nyumba kwa kutumia benki kwa kupata mkopo unaoanzia asilimia 13 mpaka 17 kwa benki nyingine na ukalipa kwa miaka kati ya 15 hadi miaka 20, hivyo ukajenga nyumba yako kwa utulivu na ukalipa kidogo kidogo badala ya kukopa kwa mtu binafsi.

“Kwa hiyo nilikuwa naomba wenzetu wa benki twende tukazungumze na watu na kuwapa taarifa, nimesikia sekta ya ukopeshaji na mabenki kwenye eneo la mkopo wa ujenzi imeongezeka na sehemu kubwa imechachushwa na wenzetu wa TMRC kwani miaka michache nyuma kwenye mwaka 2011 katika sekta ya nyumba ilikuwa kama Sh.bilioni 113.01 lakini leo hii imeongezeka mara tano kwa hiyo ni kama Sh.bilioni 531.97.

Aidha amesema Serikali itaendelea kutengeneza mazingira uwezeshi na hata mazingira tu ya kuisapoti TMRC pamoja na wadau wengine wote walioko kwenye mnyororo huo wa thamani wa nyumba.

Mgeni rasmi Kamishna wa Usimamizi wa Deni la Taifa Japhet Justin aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dk.Natu El-Maamry , akizungumza mbele ya Wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) (TMRC) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam iliofanyika jana.
OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya Kampuni ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam iliofanyika jana.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC Ndugu Oscar Mgaya akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya kuorodheshwa kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya Kampuni ya Utoaji mikopo kwa Mabenki na taasisi za fedha kwa ajili ya mikopo ya nyumba Tanzania (TMRC) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam iliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC Ndugu Oscar Mgaya mara baada ya hafla ya kuorodheshwa kwa Toleo la Nne la Hatifungani ya Kampuni ya TMRC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam iliofanyika jana.
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo

Picha mbalimbali za pamoja

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments