WAHANGA WA MAFURIKO SUMBAWANGA WAPEWA MISAADA





Kutokana na maafa yaliyo sababishwa na mvua kubwa na upepo mkali  yaliyotokea tarehe 12 /4/2023 ambayo yalisabisha vifo vya watu saba na uharibifu wa baadhi ya makazi ya wanakijiji cha Talanda kata ya Milepa halmashauri ya wilaya ya sumbawanga mkoani Rukwa.

May 7/2023 mbunge wa jimbo la Kwela Mhe. Deus Sangu  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo chakula, vifaa vya ujenzi pamoja malazi kwa wananchi walio kumbwa na mafuriko hayo.

Wakati akikabidhi msaada huo Mhe. Sangu amesema "Nimekuja hapa kutoa pole, kwanza namshukuru Mhe. Waziri mkuu kupitia kitengo chake cha maafa ametushika mkono sana katika kata hii ya milepa kwa kuleta misaada mingi ikiwepo mabati, magodoro lakini pia timu yetu ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wetu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga pamoja na Mkuu wa wilaya Sixtus Mapunda nao wamekuja kwa jitihada kubwa sana kutafuta wadau mbalimbali, na leo pia nimepokea msaada kutoka kwa wawekezaji watafiti wa gesi ya Helium waliopo ndani ya kata hii ambao ni noble Hellium Tanzania nao wamekuja kutoa mkono wa pole kwa vifaa hivyo ambavyo tumekabidhi leo. Binafsi pia nimesha wakabidhi unga mifuko 175 na ninaendelea kuwatafutia misaada kwa wadau mbalimbali, lakini jambo kubwa ambalo tunaona na fundisho kubwa linalotokana na haya maafa ni uharibifu mkubwa wa mazingira natoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza Mazingira ya safu za milima ya Lyamba lya mfipa kwa kushirkiana na TFS ambao wamekabidhiwa safu hizo."

Naye diwani wa kata ya Milepa Mhe. Apolinary Saimon Macheta amesema"Tuna washukuru sana vuongozi wa serikali ya Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga, mkuu wa wilaya Mhe. Sixtus Mapunda mbunge wa jimbo la kwela Mhe. Deus Sangu na wadau Mbalimbali kwa kuguswa na maafa haya na kuchukua hatua za dharula na kusaidia wahanga kwa kuwaletea chakula, mgadoro na mabati, tunawashukuru sana"

Aidha muwakilishi wa kampuni ya Noble hellium Bw. Edwin Mremi Inayotekeleza mradi wa utafiti wa gas ya hellium amesema "Sisi kama kampuni tumekuwa tukitekeleza shughuli zetu kwa ushirikiano mkubwa na viongozi pamoja na wananchi wa kijiji hichi cha talanda tumeguswa na maafa haya na kuona ni vyema tushiriki kwa kutoa msaada wa Unga kilo 250, maharagwe kilo 100 pamoja na sukari kilo 50 kwa familia zilizopatwa na majanga haya, lakini vilevile tumekuwa tukitoa elimu mbalimbali juu ya uharibifu na utunzaji mazingira kwa kushiriki kampeni za upandaji na uhifadhi wa uoto wa asili na mazingira. "

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Talanda ameishukuru serikali, mbunge wa jimbo la Kwela na wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa misaada  kwa wananchi waliokumbwa na adha hiyo ya maafa kijijini hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post