RIDHIWANI KIKWETE AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO CHALINZE


Na Elisante Kindulu - Chalinze

NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Ridhiwani Kikwete,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuijali Chalinze katika miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mh. Ridhiwani aliyasema hayo mara baada ya kiongozi wa mbio za mwenge kuzindua mradi wa maji wa Mdaula - Makondomengi katika Halmashauri ya Chalinze.

Mh. Ridhiwani alisema mradi huo umegharimu kiasi cha  shilingi milioni
 344 ambacho kimesaidia kuondoa tabu ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji katika maeneo hayo.

Mh. Ridhiwani ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Chalinze alisema kwamba wananchi hao walitembea umbali wa kilometa 8 kufuata maji kutoka katika maeneo wanayoishi hadi katika vyanzo vya maji.

Licha ya uzinduzi huo wa mradi wa maji , mwenge wa uhuru pia umezindua kituo Cha mabasi cha Chalinze, vipindi vya Redio vya  Chalinze FM, miradi ya madarasa katika shule ya  Sekondari ya Msata pamoja na mradi wa maabara katika zahanati ya Saleni katika Halmashauri ya Chalinze mkoani Pwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post