MIKOPO YA ZAIDI YA SH. TRILIONI 6.1 KWA WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARAMkuu wa wilaya ya Kigoma Hamis Kalli, (wa pili kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mifumo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi Being'i Issa (wa tatu kulia) akipokea zawadi wakati alipotembelea banda la Benki ya maendeleo ya wakulima(TADB) Wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sita ya mifuko ya Programu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika katika mkoa wa Kigoma.


Na Mwandishi wetu - Kigoma

Zaidi ya Mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 6.1 imetolewa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kutoka kwenye mifuko na programu sabini na mbili za uwezeshaji wananchi kiuchumi hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2023.


Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi Being’I Issa Wakati akizungumza katika Ufunguzi wa maonesho ya sita ya mifuko na Programu za uwezeshaji wananchi yanayofanyia kitaifa katika Mkoa wa Kigoma.

 ambapo amesema kuwa hizo ni Juhudi za serikali zinazofanyika kuwawezesha wananchi kujikwamua Kiuchumi ambapo mifuko hiyo ipo inayotoa mikopo ya moja kwa moja,dhamana na Ruzuku.


Bi. Issa amesema kuwa mbali na kutoa mikopo hiyo wameweza kutengeneza ajira milioni 17.6 ikiwemo wanawake milioni tisa sawa na 52%.


“Mheshimiwa Mgeni Rasmi kati ya trilioni 6.1 wanawake ni 4.7,wajasiriamali 8.6 na wanaume ni 3.9 na ajira milioni 17.6 ambapo wanawake ni milioni tisa sawa na asilimia 52%,na wanaume ni milini nane sawa na asilimia 47%”, alisema Bi Issa.


Aidha ameongeza kuwa maonesho hayo katika mkoa wa Kigoma yamelenga kukuza uelewa kwa wananchi walio wengi kufahamu huduma zinazotolewa na mifuko na programu za uwezeshaji wananchi na kuwapa wananchi hamasa ya kujiunga katika vikundi ili kuweza kunufaika.


Naye kwa upande wake Mgeni rasmi katika maonesho hayo Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ambaye aliwakilishwa na Mku wa wilaya ya Kigoma Salum kalli,akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo amesema kuwa maonesho hayo kwa mkoa wa kigoma ni fursa ya wananchi kukuza uchumi wao.


“Maonesho haya ni fursa kwetu kujifunza namna ya kuwekeza katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja,uchumi wa taasisi na Jamii”, alisema kalli na Kuongeza.


“Pia wananchi watafahamu fursa zinazotolewa na mifuko ya serikali, huduma msimbilia,huduma za kibenki,kuongeza thamani ya mazao na bidhaa,elimu ya kodielimu ya ushirika,elimu kuhusu vyama vya ushirika,elimu ya vikundi,masoko na ithibati”


Maonesho hayo yaliyoanza may 21 yanatarajiwa kufungwa may 27 na mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post