JAMAA ASABABISHA MSONGAMANO WA MAGARI BAADA YA KURUSHA MAMILIONI YA FEDHA BARABARANI


Mwanaume mmoja kutoka Oregon amesababisha msongamano wa magari kwa kurusha rundo la pesa kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi. 

Tukio hilo lilitokea kwenye barabara kuu ya I-5 mjini Eugene katika jimbo la Oregon, Marekani.

Kulingana na Fox 2, walioshuhudia tukio hilo walisimamisha magari yao na kukimbilia kuchukua kima cha $100 (KSh 13,000) zilizotawanyika kando ya barabara. 

Watu kadhaa walipiga simu kuarifu maafisa wa polisi wa Jimbo la Oregon kuhusu tukio hilo.

 Polisi waliwasiliana na mtu huyo, Colin Davis McCarthy, mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Eugene, ambaye alisema kuwa alitaka kutoa pesa hizo kama zawadi na kukadiria kuwa alitoa $200,000 sawa na takribani Milioni 460 za kitanzania

Japo hapakuwa na njia ya kudhibitisha kiasi halisi cha pesa kilichotolewa.

Ukarimu wa McCarthy ulisababisha msongamno mkubwa wa magari na hivyo kuwachochea maafisa wa usalama kumkanya kutupa pesa nje ya dirisha lake. 

McCarthy alitii na kukubali kuacha kurusha pesa barabarani. 

Jamaa wa McCarthy waliwaambia polisi kwamba hiyo ilikuwa tabia yake ya kawaida na kwamba alipata pesa hizo kwa kutumia akaunti ya benki ya pamoja ya familia yake, na kuwaacha bila senti.

"Madereva wanaosimama kando ya barabara kuu na kuingiza trafiki ya watembea kwa miguu kwenye barabara kuu huleta hatari kwa waendeshaji magari na watembea kwa miguu wenyewe," Kapteni Kyle Kennedy alisema. 

Aliongeza: “Njia za dharura zimekusudiwa kwa ajili ya dharura, hivyo kuegesha magari pembezoni mwa maeneo hayo si salama kwa ujumla, tunawaomba wananchi waepuke eneo hilo ili kuepusha hali ya hatari na pia kwa sababu hatuamini kuwa hakuna kitu kinachoweza kutokea kwa wakati huu."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments