MFUNGWA AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA KUNGUNI WENYE NJAA KALI GEREZANI


Familia moja nchini Marekani inataka uchunguzi wa uhalifu ufanyike kuhusu kifo cha jamaa wao aliyefariki akiwa jela baaa ya kudaiwa kung'atwa na kunguni.


LaShawn Thompson, 35, alipatikana akiwa amefariki katika seli chafu ya jela baada ya kuliwa akiwa hai na kunguni mnamo Septemba 2022.

Wakili wa familia hiyo alitoa picha zinazoonyesha mwili wa Thompson ukiwa umejaa kunguni. 

“Jela alilowekwa Thompson halikufaa hata kwa mnyama mgonjwa. Hakustahili kutendewa hili,” ilisoma taarifa ya wakili huyo kwa vyombo vya habari.


Kulingana na ripoti ya Mkaguzi wa Matibabu wa Kaunti ya Fulton, Thompson alipatikana akiwa hana fahamu akiwa jela miezi mitatu baada ya kukamatwa.

 Alithibitishwa kufariki kufuatia majaribio ya polisi wa eneo hilo na wafanyikazi wa matibabu kutaka kumuamsha, kwa mujibu wa ripoti ya USA Today.

 Wakili Harper anasema rekodi za jela zinaonyesha maafisa wa kizuizini na wafanyikazi wa matibabu waligundua kuwa Thompson alikuwa akidhoofika lakini hawakufanya chochote kutoa msaada au kumsaidia vinginevyo.


“Mwili wake ulipopatikana mmoja wa maafisa wa kizuizini alikataa kumfanyia CPR kwa sababu kwa maneno yake ‘alichanganyikiwa.’ Jela alilowekwa Thompson halikufaa hata kwa mnyama mgonjwa. Hakustahili hili.” 

Ripoti ya mchunguzi wa matibabu ilisema kulikuwa na “uvamizi mkali wa kunguni” katika seli yake katika wodi ya wagonjwa wa akili lakini akaongeza hakuna dalili za wazi za kuonyesha kwamba alipata mfadhaiko wa akili kwenye mwili wa Thompson. 

Picha za kutisha zilizoambatanishwa na taarifa ya Harper zinaonyesha seli ya Thompson, ambayo ni chafu mno.


Moja ya picha hizo zinamuonyesha Thompson, ambaye uso na kiwiliwili chake vinaweza kuonekana vikiwa vimefunikwa na wadudu. 

Ripoti ya mchunguzi wa afya wa Kaunti ya Fulton inaorodhesha sababu ya kifo cha Thompson kama haijabainika lakini anabainisha kulikuwa na "uvamizi mkali wa kunguni" kwenye seli yake.

 Kulingana na mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Kentucky, ambaye ni mtaalamu wa kunguni, kuumwa na kunguni kwa kawaida hakusababishi kifo.


Hata hivyo, katika baadhi ya matukio nadra, Potter alisema, kuwa katika mazingira ya mrundiko wa kunguni kwa muda mrefu kunaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini yaani anemia kali, ambayo inaweza kuwa mbaya ikiwa haitatibiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments