MREMBO AOLEWA NA JAMAA ALIYEMLEA TANGU AKIWA MTOTO MCHANGA

 Video moja imepepea mitandaoni na kuwaacha watu na hisia mseto baada ya kubainika kwamba bwana harusi alikuwa mlezi wa msichana huyo akiwa mchanga. 

Mwanamke huyu kutoka Nigeria alipepea mitandaoni baada ya kufichua jinsi alivyokutana na mumewe alipokuwa bado mtoto. 

Video aliyoshiriki kupitia akaunti yake kwenye TikTok, @iamtiwabae, ilionyesha picha yao ya zamani ya miaka iliyopita. 

Video hiyo ilifichua sherehe zao za harusi za kifahari, zikiwemo picha zao wakiwa wamevalia mavazi tofauti. 

Katika picha, mwanaume huyo alionekana akiwa amembeba mwanamke huyo, ambaye alikuwa mtoto mchanga. 

Miaka 24 baadaye wawili hao wamefunga ndoa rasmi na kuwa mke na mume. 

Video hiyo ilifichua sherehe zao za harusi za kifahari, zikiwemo picha zao wakiwa wamevalia mavazi tofauti. 


Haya ni maoni ya baadhi ya watu: @aaaaSMum alisema: "Kwa hiyo sasa umembeba mkeo, enyewe hapa ni Mungu tu." 

@Hills Judi aliandika: "Mfano mzuri wa baba utanibeba?" 

@adaobionyebuchi alisema: "Kutoka kwa yaya hadi kwa mume wa mwana." 

@Akwe Favour alitoa maoni: "Hongera kwenu." 

@Christabel Ann aliandika: "Nimechanganyikiwa." 

@Augustine precious alisema: "Hapa mimi sielewi kinachofanyika. Tafadhali naomba mtu anisaidie kuelewa maajabu haya." 

@mimi alitoa maoni: "Subiri jamani, sielewi." 

@Mideylove alitoa maoni: "Sawa... nimeelewa..." 

@Juliet Sylvester alisema: "Yuko wapi jamaa ambaye alinilea nikiwa mchanga?" 

@user9722438165070 alitoa maoni: "Nilidhani wewe ni babake." 

@Ayoyinka alisema: "Yani huyu jamaa ameona yule binti mchanga amekuwa haraka akahisi hapa hamwachi." 

@symplytianalee alisema: "Nilikimbilia sehemu ya maoni kwa sababu sielewi, nilidhani ni baba na bintiye lakini pongezi kwenu kwa kufunga ndoa."

 Itazame Video hiyo hapa: 

@iamtiwabae It can only be God #iamtiwabae #DeRealUnion #Debbieandisrael #lovestory #couple #forever ♬ Kumama Papa - Tiktok refix version - Prinx Emmanuel

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post