ABIRIA AFARIKI AKISUBIRI NDEGE UWANJANI

Polisi wanachunguza kifo cha abiria mmoja ambaye mwili wake ulipatikana eneo la kusubiri ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa akielea Mombasa usiku wa Jumamosi - Aprili 8,2023 na alikuwa amemaliza taratibu zote yarau kuabiri lakini akakosa kuelekea kwa ndege inavyohitajika. 

Wahudumu wa shirika la ndege la Jambojet waliita jina lake mara kadhaa wakimuomba kuabiri lakini hilo halikufua dafu, maafisa hao wamesema. 

Mwanaume huyo alikuwa ameketi kwenye moja ya viti katika eneo la kusubiri na aliaga dunia akiwa ameshika begi lake mkononi, kwa mujibu wa ripoti ya polisi.

Baada ya kubainika kuwa alikuwa hasongi katika kiti hicho, wahudumu wa afya wa ndege hiyo waliitwa kumhudumia na kubaini kuwa alikuwa ameaga dunia. 

Polisi wangali kubaini chanzo cha kifo hicho lakini walitaariu familia ya mwendazake huku uchunguzi ukiendelea.

 Mwili wake ulipelekwa katika hifadhi ya maiti unakotarajiwa kufanyiwa upasuaji na kupiga jeki uchunguzi wa polisi.

Via Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post