EWURA YAWABANA WAAGIZAJI, WAUZAJI NA WASAMBAZAJI WA VILAINISHI VISIVYOKIDHI UBORA



*Yawataka kusajili vilainishi vya magari/ mitambo kabla ya Mei 15, 2023.

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo uuzaji vilainishi visivyokidhi ubora katika baadhi ya maeneo nchini kinyume na sheria.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk.James Andilile imeeleza kuwa mfanyabiashara atakayekutwa na vilainishi visivyokidhi viwango atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini isiyopungua sh.Milioni kwa 10 kwa anayezalisha, milioni Saba kwa muuzaji wa jumla huku msambazaji akipaswa kulipa sh.milioni Sita na muuzaji wa rejareja sh.milioni Tano.

Aidha taarifa hiyo imesisitiza kuwa, adhabu hizo zinaweza kuambatana na vifungo mbalimbali kwa mujibu wa sheria.

EWURA imetoa onyo kwa wazalishaji, waagizaji na wauzaji wa jumla kuacha mara moja kuuza bidhaa za vilainishi vya magari/mitambo visivyokidhi ubora pamoja na kuwataka wafanyabiashara kusajili vilainishi EWURA kabla Mei 15 , 2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments