RC MNDEME AZINDUA MRADI WA MAJI KISHAPU

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akifungua maji kwenye Bomba

Na Marco Maduhu, KISHAPU

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amezindua Mradi wa Majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria wilayani Kishapu, ambao utanufaisha wananchi wa vijiji viwili vya Bupigi na Butungwa uliotekelezwa na Ruwasa wilayani humo.

Mndeme amezindua mradi huo leo Aprili 27, 2023 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambapo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana Aprili 26.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo wa maji, amewataka wananchi kuitunza miundombinu yake ili ipate kuwahudumia kwa muda mrefu, huku akiagiza Jumuiya za watumiaji maji kuhakikisha wanausimamia vizuri na kufanya matengenezo ili wananchi wasikose huduma ya maji.

Amesema Rais Samia chini ya utawala wake amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya maji, na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono katika utawala wake ili aendelee kuwaletea maendeleo.

"Kabla ya Muungano wananchi wengi walikuwa wakitumia maji ya kwenye mabwawa, visima na mito, lakini baada ya Muungano hadi sasa wananchi wanatumia maji safi na salama yakiwamo ya Ziwa Victoria, na leo tumezindua mradi mkubwa wa maji hapa Kishapu," amesema Mndeme.

Aidha, amesema katika mradi huo wa majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria ambao ameuzindua leo katika kijiji cha Bupigi ameagiza viongezwe zaidi vituo vya kuchotea maji, ili kutekekeza adhima ya Rais Samia ya kumtua ndoo kichwani Mwanamke na kumuondolea pia kupoteza muda wa kufuata maji umbari mrefu.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi wa Kishapu na Watanzania kwa ujumla, kuendelea kuuenzi Muungano kwa kudumisha Amani, upendo pamoja na mshikamano.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, amesema Serikali wilayani humo wataendelea kuuenzi Muungano,huku akimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima, amesema mradi huo wa maji Bupigi na Butungwa utanufaisha wananchi wapatao 2,000 na kuondokana na adha ya kutafuta maji umbari mrefu, huku akiahidi kutekeleza agizo la kuongeza vituo vya kuchotea maji.

Nao baadhi ya wanawake wa Bupigi wilayani Kishapu, wameipongeza Serikali chini ya Rais Samia kwa kuwatekelezea Mradi huo wa Majisafi na salama, ambao umewaondolea adha ya kutumia maji machafu na kutopoteza muda wa kufuata maji umbali mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibara wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Wiliam Jijimya akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Awali Meneja Wakala wa Majisafi na usafi wa mazingira vijijni (RUWASA) wilayani Kishapu Mhandisi Dicskon Kamanzima akisoma taarifa ya mradi huo wa maji Bupigi- Butungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akikata utepe kuzindua mradi wa maji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizindua mradi wa maji.
Mradi wa maji ukiwa umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akifungua maji kwenye Bomba mara baada ya kumaliza kuuzindua mradi huo wa maji.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akimtwisha ndoo ya maji mwanamke Rejina Maduka mara baada ya kumaliza kuzindua mradi huo wa maji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipanda mti mara baada ya kumaliza kuzindua mradi wa maji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akimkabidhi Pikipiki mwenyekiti wa Jumuiya za watumiaji maji Abedinego Joseph na kumsisitiza aitumie kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu, (kushoto) akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Wiliam Jijimya (kushoto) akiwa na Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Kamoga kwenye uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson (kushoto) akiwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kishapu kwenye uzinduzi wa mradi wa maji na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu ambayo kimkoa na kitaifa yalifanyika jana.
Muendelezo wa Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar yakiendelea wilayani Kishapu sambamba na uzinduzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.
Wananchi wakiwa kwenye muendelezo wa maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu sambamba na uzinduzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

Burudani zikitolewa kwenye muendelezo wa maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu sambamba na uzinduzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (wapili kutoka kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakifurahia burudani katika muendelezo wa maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wilayani Kishapu sambamba na kuzindua mradi wa maji.
Vijana wakiendelea kutoa burudani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akiendelea kuburudika.
Watumishi Wakala wa Majisafi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu wakipiga picha ya pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments