MTOTO ACHOMWA KISU CHA MOTO MDOMONI NA MAMA YAKE MZAZI KISA UJI


MTOTO aliyefahamika kwa jina la Martine Mihambo (6) mkazi wa Mtaa wa Ujamaa Kata ya Kalangalala Halmashauri ya Mji Geita, amedaiwa kuchomwa kisu chenye moto mdomoni na mama yake mzazi Agnesta Rubeni akidaiwa kutopeleka pesa ya uji shuleni Sh.4500.

Akielezea tukio hilo leo Aprili 6, 2023 Mama wa mtoto huyo wakati timu ya Wanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT),wakiwa na wasaidizi wa kisheria kutoka Geita, walipotembelea familia hiyo ili kuona maendeleo ya mtoto wake amesema yeye huwa ana tatizo la hasira za haraka na kuzishusha huwa ni shida, hivyo baada ya mtoto wake kumhoji juu ya pesa ambayo alitumwa kuipeleka shuleni kwa ajili ya uji Sh.4500 kuwa ameipeleka wapi kwa sababu anadaiwa, na alipogoma kumwambia ndipo akachemsha kisu jikoni na kumchoma mdomoni.


CHANZO NIPASHE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post