JK AKUTANA NA TMK WANAUME JIJINI DAR LEO


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na wasanii nguli wa Bongo Fleva wanaounda kundi la Wanaume TMK ofisini kwake Masaki jijini Dar es salaam leo, na kuzungumza nao maswala mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya sanaa.

Wasanii hao, Sir Juma Nature, Chegge Chigunda na Amani James Pausen Temba au "Mheshimiwa Temba" (kifupi Mh Temba),   wamefurahi sana kupata kile walichokiita baraka za Mzee JK wakiwa katika kukaribia kumalizia project yao ya pamoja mpya ambayo haijatajwa.

Kama itakumbukwa wasanii hao ndio waliounda kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kundi hilo lilianzishwa rasmi mnamo Septemba 16 2002 jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo "Ugali" na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni "Kutokea Kiumeni" na "Ndio Zetu". 

Wasanii wa kundi hilo kabla ya wengine kujiengua ni Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chegge, Yp, Y Dash, na wengineo.

Baada  ya kutengana kukawa na "Tmk Wanaume Halisi" na Tmk Wanaume. Tmk Wanaume likiongizwa na Mhe. Temba na Chegge wakati Tmk Wanaume Halisi kiongozi akiwa  Juma Nature na Inspector Haroun.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post