SERIKALI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU (TB)

 

Na. WAF - Dodoma 

Serikali imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau katika sekta zote ili kudhibiti na kuutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ifikapo mwaka 2030. 

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi kwenye kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara kilichofanyika katika ofisi za Waziri Mkuu Jijini Dodoma. 

“Ili kudhibiti ugonjwa huu wa Kifua Kikuu ni muhimu kushirikiana na wadau wengi kama sekta ya afya, wadau sekta ya elimu, sekta ya usafirishaji na sekta nyingine mbalimbali.” amesema Dkt. Yonazi

Kwa upande wake Mtaalamu Mshauri kutoka Stop Tb Partnership (STP) Bw. Oscar Mukasa wakati akiwasilisha taarifa ya mpango kazi wa kudhibiti Kifua Kikuu amesema watu wenye hatari zaidi ya kupata Kifua Kikuu ni pamoja na watu wanaoishi kwenye makazi duni, Watoto, Wavuvi na Wanaoishi Bweni. 


Pia, amesema Watu wenye VVU, watu wenye Utapiamlo, wachimbaji madini, wanaoishi na mgonjwa wa Kifua Kikuu, watoa huduma za afya na wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano. 


Mwisho, Bw. Mukasa amewashauri wanaoishi katika mazingira hayo kuchukua tadhari  za kujikinga na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments