KATIBU MKUU CCM AINGILIA KATI MGOGORO WA MIPAKA KATI YA HIFADHI YA TARANGIRE, VIJIJI TISA,ATOA MAELEKEZO KWA WAZIRIKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii au wataalamu wake kwenda kushughulikia mgogoro wa mpaka kati ya vijiiji tisa na Hifadhi ya Tarangire mkoani Manyara.


Chongolo ametoa maagizo hayo leo Machi 7,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Magala ambapo akiwa hapo Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Siro alitoa kero hiyo ya mgogoro wa mipaka kwa niaba ya wananchi.Mgogoro unahusisha mipaka kati yao na Hifadhi ya Tarangire.


"Namuagiza Waziri aje haraka yeye au wataalamu wake wapitie waangalie uhalisia wa mipaka hii baadae wazumgumze na wananchi kwenye vijiji vilivyopo pembezoni na kisha wawaambie ukweli kama mna haki na kama hamna haki muambiwe.

"Huo ndio uungwana ,wananchi hamuwezi kuwa mnalalamikia jambo kwasababu hamjui nani mwenye haki ,wakija wenyewe watakaa na ninyi wataonesha walipoweka mipaka hiyo na ikithibitika mipaka hiyo ni halali ,si mnaacha mnaendelea na mambo mengine , sasa waje hapa na ndio wajibu wa viongozi,"amesema Chongolo.


Ameongeza kwamba kazi ya kiongozi sio kukaa ofisini bali ni kutoka na kwenda kuwatumikia wananchi na huo ndio wajibu wa msingi na sio vinginevyo."Sisi wote tumepewa dhamana ya kumsaidia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.


"Mawaziri wako chini yangu na nimi nawanyooshea vidole wewe pale hujaenda sawa ,hapo hujaenda sawa na wao wajibu wao ni kuhakikisha wanawanyooshea vidole wa chini yao ili tutafute tija ambayo tumeahidi kwa wananchi na sio vinginevyo ,imani inazaa imani na sio vinginevyo.
"Rais amewapa imani ili wao imani hiyo wailazishie imani nyingine wananchi na mimi nikishamwambia Waziri atakuja, kwani najua anapenda kazi, najua atakuwa mtu wa kwanza kuja ,akichezea kitumbua kitaingia mchanga .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post