MBUNGE DITOPILE AFUTURISHA DODOMA, WAMUOMBEA DUA RAIS SAMIA

Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile ameandaa Iftari na Dua Maalum ya Watoto Yatima na Wajane kuiombea Nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Hafla hiyo ya Iftari imefanyika katika Hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma ambapo Mgeni wa Heshima alikuwa ni Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini David Kihenzile.


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments