WANAWAKE TUME YA UCHAGUZI WATOA MSAADA GEREZA KUU ISANGA DODOMA


Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuwia Sultan (kulia aliyeshika boksi) akikabdhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Msaidizi wa Gereza la Wanawake Isanga, Mrakibu Msaidizi wa Magereza Yuster Ligazio wakati wanawake watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi walipowatembelea Gereza Kuu Isanga Dodoma na kukabidhi msaada huo kwaajili ya wafungwa, mahabusi wanawake na watoto wao katika Gereza hilo. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa Duniani kote Machi 8 ya kila mwaka.
Wanawake watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa na Maafisa Magereza baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya wafungwa, mahabusi wanawake na watoto wao katika Gereza Kuu Isanga jijini Dodoma. Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa Duniani kote Machi 8 ya kila mwaka.
Wakitoka kusalimia wafungwa wanawake na mahabusi katika gereza la wanawake. --

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post