MHUNI ALIYEJIFANYA MWANAMKE NA KUTAPELI AKAMATWA


Maafisa wa polisi wamemkamata mwanaume aliyekuwa akijifanya mwanamke katika soko la Bomet nchini Kenya.

Katika video iliyopakiwa kwenye TikTok na Noah Kips, mwanaume huyo alikuwa amevaa wigi iliyomfanya aonekane kama mwanamke.

Pia alikuwa amevaa sidiria ambayo aliitoa baada ya maafisa wa polisi kumvamia. 

Maafisa hao wa polisi pia wanaonyeshwa wakimshurutisha kijana huyo kuvaa wigi lake vizuri na sidiria ili kumpa mwonekano mzuri wa kike.

"Weka wigi lako hivi ili uonekane mwanamke. Chukua sidiria yako uvae na weka mifuko ya kazi ndani kama kawaida, iweke jinsi ilivyokuwa ili tukusamehe," maafisa hao walimwambia mwanamume huyo.

Kama inavyoonekana kwenye video, kijana huyo hakuwa na budi ila kufanya kama maafisa walivyoamuru. Hivyo, alitoa fulana yake ya pinki na kuvaa sidiria yake tena. Maafisa wa polisi walibaki wakishangaa na kumuuliza kwa nini alijifanya mwanamke.

"Nia yako ilikuwa nini?" polisi mmoja alisikika akimuuliza lakini hakujibu. Maafisa hao walisikika wakimuuliza mwanamke aliyekuwa na mwanamume huyo sokoni iwapo alijua alikuwa mwanamume. Lakini mwanamke huyo alikana. “Sikujua, sisi sote tunauza bidhaa zetu hapa,” alisikika mwanamke huyo akimjibu afisa huyo
@noahkips

♬ original sound - NOAH Kips

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments