CRDB YAENDESHA SEMINA YA HUDUMA YA BENKI MTANDAO KWA WATEJA WAKE WAKUBWA KANDA YA MAGHARIBI MKOANI SHINYANGA

Benki ya CRDB ikitoa Semina kwa wateja wake wakubwa Kanda ya Magharibi Mkoani Shinyanga juu ya huduma ya Benki Mtandao.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BENKI ya CRDB imeendesha Semina ya huduma ya Benki Mtandao (Internet Banking), kwa wateja wakubwa Kanda ya Magharibi mkoani Shinyanga ili kuzifahamu huduma hizo na kuzitumia.

Semina hiyo imefanyika leo Machi 13, 2023 Mjini Shinyanga.

Meneja wa Benki Mtandao Sarah Nzowa akizungumza kwenye Semina hiyo, amesema ni endelevu kwa wateja wao wakubwa ili wazifahamu huduma hizo ambazo zitawapunguzia gharama mbalimbali za kwenda kupata huduma kwenye Tawi.

Amesema mteja akitumia huduma ya Internet Benki itamrahisishia kutoa huduma haraka kwa watumishi wake ikiwamo malipo ya mishahara, kuokoa gharama za usafiri kwenda kupata huduma kwenye Tawi, na gharama za Stationary kwa sababu huduma hizo za mtandao hazitumii makaratasi.

“Huduma za Benki Mtandao kutoka CRDB ni nzuri sana kwanza kuna usalama wa fedha, na pia unaweza kutuma pesa kwenda nje ya nchi, na unapata huduma muda wote masaa 24 tofauti na kwenye Tawi ambapo siku za wikiendi na sikukuu huwa hakuna huduma lakini Internet Benking huduma ni masaa yote,”anasema Nzowa.

Naye Meneja Mahusiano kutoka Benki ya CRDB Mbutolwe Mwaipopo amesema huduma hiyo ya Benki Mtandao ina faida sana kwa wateja wakubwa hasa kwenye malipo ya Mishahara kwa sababu ukilipa Mshahara kupitia huduma hiyo kwa kila Mtumishi unakatwa Sh.1,999 lakini kwa mfumo wa kawaida ni Sh.3,500.

Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga George Nyegu ambaye ni Meneja huduma kwa wateja, amesema huduma ya Benki Mtandao ni nzuri, kwa sababu kuna baadhi ya wateja wanakwenda kwenye Tawi kupata huduma wakati muda wa kazi ukiwa umekwisha, lakini wakiwa na huduma hiyo ni kupata huduma muda wote na kutoa wito kwa wateja wa benki hiyo wajiunge na huduma ya Internet Benking.

Nao baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB ambao wanatumia huduma ya Benki Mtandao, wamesema wanafaidika sana kwa kupata huduma zote za kibenki mtandaoni na kwa wakati ikiwamo kulipa mishahara watumishi wao.

Kwa upande wa wateja ambao hawakuwa wakitumia huduma hiyo, wamesema baada ya kupata Semina wataanza kuitumia, kwa sababu wameona inafaida kubwa ikiwamo kuokoa gharama na kutopoteza muda wa kwenda kwenye Tawi bali huduma zote zinapatikana mtandaoni.

Kaimu Meneja wa Benki ya CRDB Mkoa wa Shinyanga George Nyegu akizungumza kwenye Semina ya huduma ya Benki Mtandao kwa wateja wao wakubwa Kanda ya Magharibi mkoani Shinyanga.

Meneja Biashara Kanda ya Magharibi kutoka Benki ya CRDB Dionis Mambo akizungumza kwenye Semina ya huduma ya Benki Mtandao kwa wateja wao wakubwa Kanda ya Magharibi mkoani Shinyanga.

Mtaalamu wa Mfumo wa Benki Mtandao kutoka CRDB Emmanuel Makoye akitoa elimu ya huduma ya Benki Mtandao kwenye Semina hiyo.

Meneja wa Benki Mtandao kutoka CRDB Sarah Nzowa akitoa elimu ya huduma ya Benki Mtandao( Internet Banking) kwa wateja wakubwa wa Benki hiyo Kanda ya Magharibi Mkoa wa Shinyanga.

Meneja Mahusiano kutoka Benki ya CRDB Mbutolwe Mwaipopo akitoa elimu na faida ya kutumia huduma ya Benki Mtandao kwenye Semina hiyo.

Wateja wakubwa wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi mkoani Shinyanga kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa kwenye Semina ya Benki ya CRDB ya huduma ya Benki Mtandao.

Semina ya huduma ya Benki Mtandao kutoka CRDB ikiendelea.

Mteja wa Benki ya CRDB Kheri Ndaki akielezea namna walivyonufaika na Semina hiyo na kuahidi kuendelea kutumia huduma ya Benki Mtandao.

Mteja wa Benki ya CRDB Mercy Athanas akielezea namna anavyonufaika na huduma ya Benki Mtandao.

Mchungaji Odolous Gyunda kutoka (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, akitoa Pongezi wa Semina hiyo ambayo itawasaidia katika matumizi ya huduma za kifedha kupitia huduma ya Benki Mtandao.
Katibu Mkuu wa KKKT Happines Gefi akielezea namna walivyonufaika na Semina hiyo ya huduma Benki Mtandao kutoka CRDB.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa Semina ya huduma ya Benki Mtandao kutoka CRDB.

Viongozi kutoka CRDB wakipiga Picha ya Pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments