SHIRECU YAENDESHA MKUTANO MKUU WA 28, ‘GINERY’ KUFUFULIWA, DC JOHARI ATAKA USHIRIKA UINUE UCHUMI WA WANANCHIMkutano Mkuu wa 28 wa Chama Kikuu Cha Ushirika (SHIRECU).

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA Kikuu cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU), kimeendesha Mkutano Mkuu wa 28, kwa kujadili mambo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirika, huku Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitaka ushirika uinue uchumi wa Wananchi.

Mkutano huo umefanyika leo Machi 10, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Chama hicho mkoani Shinyanga na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwamo na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme

Mwenyekiti wa SHIRECU Kwiyolecha Nkilijiwa akisoma taarifa kwa wajumbe wa Mkutano huo, amesema SHIRECU kwa sasa inazaliwa upya, ambapo wamejiwekea malengo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo kufufua ‘Ginery’ za kuchakata mazao, kuongeza vyanzo vya mapato na kupunguza madeni.

“SHIRECU itarudi kileleni ikiwa sisi sote tutazungumza lugha moja, mipango mikakati tuliyonayo ni kufufua ‘Ginery’ ya Mhunze pamoja na kusimika Mashine ya kukoboa zao la dengu Kanda ya Solwa na kuhamisha Less kutoka Uzogore kwenda Solwa,”amesema Nkilijiwa.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, akizungumza kwenye Mkutano huo, amesema Vyama Vikuu vya Ushirika vinapaswa kufufuliwa na kushikwa mkono na Serikali pamoja na kupewa mitaji ili vianze kununua mazao na kuchakata na kujiendesha kwa faida.

Naye Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Shinyanga Christina Mzava, amesema SHIRECU mpya Irejee ili iendelee kuwa mkombozi kwa Mkulima, huku akiwataka mikopo ambayo wamekuwa wakikopa zitekeleze malengo yaliyokusudiwa, pamoja na kuacha kuzalisha madeni ambayo hayana tija.

“SHIRECU mlikuwa na madeni makubwa lakini sasa hivi mmeanza kuyapunguza hii ni hatua nzuri na msikubali kuendelea kuzlisha madeni ambayo hayana tija, na mikopo ambayo mnakopa isi ishiye kwenye shughuli za uendeshaji tu, bali iwaguse na Wakulima kwa kuwawezesha ili wafanye Kilimo cha kisasa na Kilimo Biashara.

Aidha, ameviomba pia vyama vya Msingi vya Ushirika viache tabia ya kukopa wakulima pale wanapokuwa wakiuza mazao.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amevitaka vyama vya ushirika vitekeleze majukumu yao ipasavyo kwa kujiimarisha pamoja na kuinua uchumi wa Mwananchi.

Nao baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo akiwamo Albert Kapongo, wamesema mambo ambayo yamekuwa yakihusu Chama wawe wanashilikishwa hasa kwenye jambo la upangishaji jengo la makao makuu (SHIRECU) kwa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Tawi la Shinyanga sababu wao ndiyo wenye mali.

Katika Mkutano huo pia iliwasilishwa Taarifa ya ukaguzi ya vyama vya Ushirika kutoka (COASCO).

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa akizungumza kwenye Mkutano wa 28 wa (SHIRECU).

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) Kwiyolecha Nkilijiwa akizungumza kwenye Mkutano wa 28 wa (SHIRECU).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava akizunguma kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Bonipahce Butondo, akizunguma kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Naye Mkaguzi wa vyama vya Ushirika mkoani Shinyanga (COASCO) Rodrick Kilemile,akizunguma kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Makamu Mwenyekiti wa (SHIRECU) Josephat Limbe akizunguma kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava, (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Christina Mzava (kulia) akiwa na Diwani wa Iselamagazi Halmashauri ya wilayani Shinyanga Izack Sengerema kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kushoto) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama Kikuu cha Ushirika (SHIRECU) ukiendelea.

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU) Charles Shigino akichangia Mada kwenye Mkutano huo.

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa (SHIRECU).

Mjumbe akichangia Mada kwenye Mkutano huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post