MME ADAIWA KUMUUA MKEWE KISHA KUMZIKA CHUMBANI CHINI YA KITANDA TABORAShimo chumbani alimofukiwa marehemu

Mwanamke aitwaye Salma Maulid mkazi wa Mtaa wa Mbilani Kata ya Kidongo Chekundu Manispaa ya Tabora, ameuawa na mtu anayedaiwa kuwa ni mumewe kisha mwili wake kufukiwa chumbani, chini ya uvungu wa kitanda.


Tayari mwili wa marehemu umefukuliwa na Jeshi la Polisi limetangaza kumsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye alitoweka kusikojulikana baada ya kutekeleza tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi.


Amesema mtuhumiwa baada yakutekeleza tukio hilo amekimbia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post