PINDA ATAKA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA KUONGEZA MADUHULI YA SERIKALI


Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiongea na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akiteta na jambo na Makamishna wa Wasaidizi wa Ardhi Nchini mapema leo Jijini Dodoma.
Makamishna Wasaidizi wa Ardhi Nchini wakifuatilia jambo leo Jijini Dodoma katika Kikao Kazi kilichowakutanisha pamoja ili kujadili namna bora ya ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la Ardhi.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Geofrey Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara pamoja na Makamishna Wasaidizi wa Ardhi mara baada ya kufunga kikao kazi na viongozi hao Jijini Dodoma.

Na: Anthony Ishengoma- Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Bw. Makazi Geofrey Pinda amesema vipaumbele vya Wizara kwa sasa ni kuongeza kasi ya ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia pango la Ardhi lakini kuboresha mawasiliano kati ya watendaji ardhi walioko katika Ngazi ya Halmashauri.

Naibu Waziri Pinda amesema kuna changamoto ya mawasiliano kati ya watendaji Sekta ya Ardhi walioko katika Halmashauri mbalimbali nchini kwani wengi wamekuwa wakiwajibika kwa mamlaka za Serikali za Mitaa badala ya Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa na kusahau kuwa mwajili wao ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi.

Naibu Waziri Pinda amesema kwa muda mfupi tu aliokaa Wizarani amegundua kuwa kuna changamoto hiyo kutokana na mamka za kupanga na kumilikisha ardhi kuwa katika Halmashauri husika wakati mwajili wa wataalam hao ni Wizara ya Ardhi jambo lilopelekea uwepo kwa changamoto hii.

Pinda amesema hayo mapema Jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Anthony Sanga pamoja na Makamishna Waasaidizi wa Miko na Waratibu Mikoa ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka viongozi hao kuwasilisha maoni ili sheria ya ardhi iweze kuboreshwa katika mapitio ya sheria yaliyoko kwenye mchakato.

Aidha Naibu Waziri Pinda amesema ipo haja ya kupitia muhundo upya wa watumishi hao ili ikiwezekana waweze kuwajibika kinidhamu kwa Kamishna Msaidizi wa Mikoa ili kuongeza uwajibikaji kiutendaji ili kusaidia Kamishna huyo kutekeleza kazi zake ipasavyo.

Suala lingine alilogusia kiongozi huyo nikuhimiza uwajibikaji wa pamoja wa watumishi walioko katika ofisi za mkoa bila kujali kada zao kwani wote kwa pamoja wanafanya kazi katika Sekta ya Ardhi hapa Nchini.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga aliwambia watendaji hao kuwa kipaumbele chake ni kuongeza makusanyo ya kodi ya ardhi na kwamba yeye kila atakapita katika Ofisi za Ardhi Mkoa ataomba kupatiwa takwimu za makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Sanga ameongeza kuwa tayari timu ya wataalam wa Tehama na wengine wako kazini kutengeneza mfumo mpya na rafiki utakaowawezesha watanzania kulipa kodi ya ardhi kupitia miamala ya simu tofauti na sasa ambapo wananchi wanalazimika kupanga foleni katika Ofisi za Wizara Mikoani kwa ajili ya kulipa kodi.

Eng. Sanga amewataka waratibu wa Kodi Mikoani kote kuwa na takwimu sahihi za walipa kodi ikiwemo kuwatambua wote ikiwemo wale ambao hawajarasimisha ardhi yao ili waweze kuingiza katika mfumo wa walipa kodi kama ilivyo katika miamala ya Mamlaka za maji hapa Nchini.

Eng. Sanga amesema timu ya wataalam tayari iko kazini ikifanyia kazi mfumo wa ukusanyaji mapato ambao utakuwa ni wa aina moja nchi nzima tofauti na sasa ambapo mifumo ya ukusanyaji mapato inatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine suala ambalo amesema litaongeza kasi ya makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia Pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi anakutana na Makamishna wa Ardhi Nchini pamoja na Waratibu wa Kodi kutoka Ofisi za Wizara ya Ardhi walioko mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kupeana taarifa likini pia kukumbushana masuala muhimu ikiwemo yatakonayo na Mkutano wa awali uliowakutanisha mjini Morogoro hivi karibuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments