RC KINDAMBA AANZA KAZI RASMI TANGA...AZITAKA HALMASHAURI KUONGEZA JUHUDI UKUSANYAJI WA MAPATO

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akipokelewa rasmi na viongozi mbalimbali mkoani Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akipokelewa rasmi na viongozi mbalimbali mkoani Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza na viongozi mbalimbali Mkoani Tanga


Na SALMA AMOUR, TANGA

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewataka watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali kufanya kazi kwa weledi na juhudi katika kukuza uchumi wa Tanga ili kuleta maendeleo kupitia ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zote 11 ili kuufanya mkoa huo kukua katika ngazi za Taifa kwa ujumla .


Akizungumza mara baada ya kupokelewa na watumishi wa umma, wakurugenzi wa wilaya na Makatibu tawala ikiwa ndiyo mara ya kwanza kuwasili Mkoani Tanga tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutumikia wananchi wa Tanga mkuu wa mkoa huyo amebainisha kuwa ili maendeleo yaweze kuonekana ni lazima kuwe na viongozi bora watakaoshikilia usukani wa kuleta mabadiliko ikiwemo ukusanyaji wa mapato ambayo ndio lango kuu la kukuza uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo ipasavyo ikiwemo miradi ya elimu, afya, maji na mengineyo.


"Niwaombe tu viongozi na watumishi kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato katika kuimarisha mkoa wetu kuwa ni mkoa wa maendeleo, na imani ili suala mutaweza kulipokea na kulifanyia kazi kuanzia sasa, wananchi wana hamu ya kuona matokeo mazuri ya Mabadiliko kwenye ngazi tofauti tofauti za kiutendaji na sio vinginevyo", alisema Waziri Kindamba.


Aliongeza kuwa Ili kuleta mabadiliko kwa kufikia lengo ni lazima viongozi washirikiane bega kwa bega katika mambo muhimu ya kuiboresha mkoa huo kuwa na maendeleo.


"Mpaka kufikia Sasa mkoa wa Tanga umekusanya asilimia 56 za mapato ili kuweze kufikia lengo ni lazima kufanye kazi kwa bidii ili tufikishe asilimia 100 ambapo tutakuwa kumeshafikisha lengo kwenye Jiji letu ya Tanga", alisisitiza Waziri Kindamba.


Kwa upande Wake Katibu Tawala Tanga Pili Mnyema ameahidi kutoa ushirikiano na viongozi wengine katika kuleta Mabadiliko ya kimaendeleo kwa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ya maendeleo kwa Taifa.


" Ninaahidi Mimi pamoja na watumishi wenzangu na viongozi wa taasisi mbalimbali ambao wako kwenye jiji letu la Tanga kuwa tunaendelea kushirikiana na kupambana kwa pamoja kwenye mambo mbalimbali ya kutuletea mabadiliko,kama ambacho serikali yetu ilivyotuamini basi hatuna budi kuidumusha imani hivyo kwa kutenga yake wenye msingi lakini pia nikutue hofu mkuu wa mkuu kuwa Tanga ndio Mama wa ukusanyaji wa mapato tutapambana vyema katika kuhakikisha kuwa halmashauri zote zilizopo zinafsnya vizuri.


Aidha Waziri Kindamba amewataka wanaohusika katika usimamizi wa miradi mbalimbali kuenda na muda husika ili kuepusha ukwamishaji wa kuleta maendeleo na mabadiliko kwa muda husika uliopangwa.

"Tusisubiri mpaka viongozi wa kitaifa kuja kutukosoa, tunatakiwa sisi wenyewe kukaguana katika kutekeleza shughuli za kuleta maendeleo kwenye jamii yetu ili tuwe mfano mzuri katika mikoa mingine waweze kuiga namna ya uendeshaji wa shughuli zetu.


Katika hatua nyingine amelitaka Jeshi la polisi kutoa kipaumbele katika kupambana na watu wanaokiuka sheria za nchi kwa kwa kujihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambazo zinaathiki vijana wengi mkoani hapo ikiwa ndio nguvu kazi ya Taifa.


"Niwaombe Jeshi la polisi kuwa macho wakati wote na kufuatilia kwa umakini walee wote wanaouza,wanaotumia dawa za kulevya kuchukuliwa hatua za kisheria ili kuwanusuru vijana wetu katika mambo yasiyofaa na pia kuendelea kupambana na watu wakaidi ambao wanafanya vitendo kwa ukatili wa kijinsia kwenye jamii yetu suala la ulawiti, ubakaji na ushoga limekuwa gumzo hatarishi katika jiji hili ikawa niwapongeze jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali ambapo Hali ni nzuri  kwa sasa lakini pia matukio kama haya bado yapo", alisema.

*********

MWISHO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments