MHUBIRI ALIYEFARIKI MWAKA 2021 NA KUSUBIRIWA AFUFUKE HATIMAYE AMEZIKWAMhubiri ambaye alifariki mwaka 2021 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini na mwili wake kuhifadhiwa na kuombewa akitarajiwa kufufuka hatimaye amezikwa.

Mwili wa pasta wa Gauteng - Siva Moodley - umekuwa katika makafani ya Johannesburg tangu Agosti 15, 2021 alipokumbana na mauti.

Mwanzilishi huyo wa kanisa la The Miracle Centre lililo kaskazini mwa Johannesburg aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kuwa mgonjwa. 

Kwa mujibu wa ripoti ya awali ya jarida la OIL, familia ya Mooley na washirika wake wamekuwa wakizuru makafani hayo kusali ili afufuke.

Licha ya haya, meneja wa makafani hayo Martin du Toit aliwasilisha ombi katika mahakama ya Johannesburg akitaka ruhusa ili auzikwe au kuuchoma mwili wa Moodley. 

Tangu kufa kwake, inaarifiwa ibada zimekuwa zikiendelea katika kanisa lake, zikiendeshwa na mke wake Jessie, na wanawe wawili David na Kathryn Jade. 

Ibada hizi hupeperushwa moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo inaarifiwa kuwa kanisa halijakiri kufariki kwa mhubiri huyo.

Kutokana na hilo, inadaiwa halijatangaza kifo chake kwenye mitandao ya kijamii wala kuwaambia washirika aliko pasta wao.

 Pia imearifiwa kuwa akaunti za Moodley kwenye mitanao ya kijamii - hususan Facebook na Twitter - bado zinafaya kazi na jumbe kuanikwa hapo kila siku kanakwamba zinatoka kwake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments