VIJANA WA ULINZI SHIRIKISHI WAONYWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIHALIFU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala liwewaonya baadhi ya vijana wa ulinzi shirikishi kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya kihalifu wakati wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi katika mitaa yao.Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Dr. Debora Magiligimba ACP katika bwalo la Polisi Buguruni alipokutana na vijana wa ulinzi shirikishi katika Wilaya ya Kipolisi Buguruni kwa lengo la kuwapa maelekezo na mwongozo wa utakaosaidia kuboresha utendaji wa kazi za ulinzi shirikishi katika maeneo yao.


 "Baadhi ya vijana wa ulinzi shirikishi mmekuwa mkishirikiana na wahalifu kwani mnatoa taarifa ya doria zenu kwa wahalifu mkiwajulisha sehemu mlipo jambo ambalo linawasaidia wahalifu hao kujipanga na kubadili sehemu ya kwenda kufanya matukio ya uhalifu",amesema.


Pia Kamanda Dr. Debora Magiligimba ametaka kila kikundi cha ulinzi shirikishi kuhakikisha kunakuwa na sare kwa ajili ya kuvaa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ya ulinzi katika mitaa yao.


" Sare zinasaidia kuwatofautisha na vibaka pindi uhalifu unapotokea jambo ambalo litawasaidia wananchi kuwatofautisha na wahalifu", ameongeza.


Aidha Kamanda Dr. Debora Magiligimba amewataka vijana hao wa ulinzi shirikishi kuepuka vitendo vya ukatili katika familia zao na kutoa rai kwao kama kuna kijana wa ulinzi shirikishi ametendewa matendo ya ukatili wawezekufika katika madawati ya kijinsia na watoto yaliyopo katika vituo vya Polisi kutoa malalamiko yao.
Kikao hicho cha ulinzi shirikishi kiliudhuriwa Wakaguzi Kata 08 na vijana wa ulinzi shirikishi wapatao 139 kutoka katika Kata 08 zinazopatikana katika Wilaya ya Kipolisi Buguruni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments