IDADI YA WATU WALIOFARIKI KUTOKANA NA TETEMEKO YAFIKIA 5000 UTURUKI


Idadi ya vifo inaongezeka hadi sasa zaidi ya 5,000 vimerekodiwa kutokana na tetemeko lilitokea siku ya jumatatu.


Nchini Uturuki, idadi ya watu ambao wamekufa kwa sababu ya matetemeko haya ya ardhi imeongezeka hadi 3,381, kulingana na mamlaka ya maafa nchini humo.

Orhan Tatar, afisa katika Mamlaka ya Usimamizi wa Maafa na Dharura (AFAD), anasema wengine 20,426 wamejeruhiwa na majengo 5,775 yameporomoka.

Hesabu hiyo mpya inafikisha idadi ya waliofariki nchini Uturuki na nchi jirani ya Syria kufikia 4,890. Idadi hii huenda ikazidi kuongezeka.Tetemeko jipya la ardhi lenye nguvu limeripotiwa katikati mwa Uturuki.

Utafiti wa Jiolojia kutoka Marekani unasema tetemeko lenye ukubwa wa 5.5 lilikuwa katika kina cha kilomita 10 (maili 6) karibu na mji wa Golbasi.

Wakati huo huo, Kituo cha Ulaya-Mediterranean Seismological Center (EMSC) chenye makao yake nchini Ufaransa kiliweka nguvu ya tetemeko kuwa karibu na Golbasi 5.6, na kuongeza kuwa lilikuwa katika kina cha 2km.

Mashirika yote mawili yalisema tetemeko hilo lilitokea saa 03:13 GMT siku ya Jumanne. Hawakutoa maelezo zaidi.

Eneo la Kusini-mashariki mwa Uturuki limekumbwa na mfululizo wa mitetemeko kufuatia tetemeko kuu la ardhi karibu na mji wa Gaziantep Jumatatu asubuhi.

endelea kuwa nasi kwa matukio yote ya hivi punde.


Via: BBC

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post