RAIS SAMIA ATANGAZA KUNUNUA KILA BAO LA SIMBA, YANGA



Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya kununua kila goli kwa Tsh. Milioni 5/- wakati timu za Simba na Yanga zikicheza michezo yao Kimataifa dhidi ya timu kutoka nje ya nchi, wikiendi hii.

Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kuwa, Dkt. Samia anatambua umuhimu wa michezo nchini, hivyo ametoa ahadi hiyo kuzipa hamasa timu hizo mbili za Simba SC ambao wanashiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga SC ambao wanacheza Kombe la Shirikisho barani Afrika.

“Rais wetu anatambua umuhimu wa michezo nchini, hivyo ametoa hamasa hiyo wakati timu zetu zikicheza Michuano hiyo ya Kimataifa wikiendi hii (Jumamosi na Jumapili), sasa ni kazi kwa Wachezaji wa Simba na Yanga kufunga mabao ya mengi ili kuweiweka Tanzania katika nafasi nzuri katika mashindano hayo”, amesema Msigwa.

“Wachezaji wa Yanga na Simba sitaki kutaja majina hapa kazi kwenu, ukifunga mabao 10 una Milioni 50, ukifunga mabao 20 una Milioni 100, ukifinga mabao mawili una Milioni 10, lakini lengo la Mhe. Rais ni kuhakikisha timu zetu zinashinda kwenye mashindano hayo yanayowakilishwa na timu za mataifa mbalimbali barani Afrika”, ameeleza Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema, Dkt. Samia anatambua umuhimu wa michezo nchini Tanzania katika kuitangaza nchi sanjari na kuimairisha tasnia ya burudani kwa kutoa mikopo kwa Wasanii mbalimbali ili kuwapa nafasi Wasanii hao kuendelea kazi zao za sanaa kwa maendeleo ya taifa.

Simba na Yanga zitakuwa kibaruani wikiendi hii kupeperusha bendera ya taifa la Tanzania katika mashindano ya Kimataifa, Simba SC watacheza na Raja AC, Februari 18, 2023 wakati Yanga SC wakicheza Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe, Februari 19, 2023.


Chanzo - Michuzi Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments