BABU ANYOFOLEWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI, MWILI WAKE WATUPWA ZIWA VICTORIAMtu moja aliyetambulika kwa jina la Musa Robert anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 76 mkazi wa Kijiji cha Kasheka kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amekutwa amefariki dunia pembezoni mwa ziwa Victoria katika kitongoji cha Kisenya Kijiji cha Katwe kata ya Katwe wilayani humo huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.


Ofisa mtendaji Kijiji cha Katwe, Ezekiery Galula akizungumuza na Mwananchi February 12, 2023 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeleta simanzi kwa wananchi wa maeneo hayo.


Amesema alipata taarifa kutoka la raia wema waliopita maeneo hayo wakiwa wanakwenda kufanya shughuli za kujipatia kipato ndipo walipoona mwili huo na kutoa taarifa.


Mdogo wa marehemu Manyindo Robert (74)  amesema sehemu za siri kwenye mwili wa marehumu kaka yake zilikuwa zimenyofolewa na hazijulikani zilipo licha na viungo vingine kuwepo.

Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post